Serikali 1, 2 au 3 - Nukuu kutoka kwa Mwalimu Nyerere

Serikali 1, 2 au 3 - Nukuu kutoka kwa Mwalimu Nyerere

Maishamapya

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
1,279
Reaction score
375
Sasa hivi hoja inayotawala ni juu ya hotuba ya Jaji Warioba na jinsi alivyojega hoja za nguvu kuhusu haja ya kuwa na Serikali 3 kwa sasa na hasa ikizingatiwa ya kwamba Katiba ya Zanzibar imevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wana-CCM wameruhusu Katiba Kuvunjwa na sasa wanataka kushinikiza serikali 2 bila kurejea pale walipokosea. Hii inanikumbusha pal Mwalimu alipoandika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=9489&d=1271349502). Nimedondoa nukuu kadhaa ili kujikumbusha na kujiuliza: Je, mkakati wa sasa wa wanaccm kuzuia serikali 3 utafanikiwa hasa ukizingatia kuwa katiba ya JMT imevunjwa? Ili kurekebisha hilo basi ni lazima wazanzibari warekebishe katiba yao - Je, CCM Zanzibar watapata 2/3 ya kura kufanyia marekebisho hayo?

Nukuu Zenyewe hizi hapa:

[TABLE="width: 738"]
[TR]
[TD]Mambo ya Muungano - Nukuu kutoka kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania ( 2010 Edition)
[/TD]
[TD]Uk
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mapatano hayo yalifanywa kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania. Hilo halina ubishi. Miungano mingi ya aina hii duniani, imefanywa na viongozi kwa njia hii au nyingine kwa niaba ya wananchi, bila kuhojiwa na hapana sababu ya kuhojiwa kitendo hicho. Kwa msingi huo wale wachache wanaohoji na kutaka kura ya maoni juu ya suala hili, hawaitakii mema nchi hii. Hoja hiyo haikubaliwi na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
[/TD]
[TD]9
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mheshimiwa Spika, tangu kuanzishwa kwa Muungano wa nchi zilizokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya watu wa Tanganyika, ziliungana na kuwa nchi moja na Taifa moja. Narudia tena, ziliungana kuwa nchi moja na Taifa moja. Kwa lugha ya kigeni, 'One Sovereign State'. Hivyo imejenga msingi imara wa umoja kati ya wananchi wa Tanzania. Tanzania Bara na Visiwani, zimekuwa zikifaidika kisiasa, kiuchumi na kiulinzi chini ya mfumo uliopo waMuungano. (Makofi)
[/TD]
[TD]9
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wazee hawa waliendelea kuja kuniona au Msasani au Butiama baada ya suala la Zanzibar kuingia katika OIC lilipozuka. Hili nalo viongozi wetu wakaliombea bungeni, na wakapewa muda wa mwaka mmoja wa kulitafakali! Suala la kuvunja Katiba ya Nchi yetu!
[/TD]
[TD]16
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Siku hiyo baadhi ya wabunge, viongozi wa hoja ya Serikali Tatu, waliomba kuja kuonana name Msasani. Tulizungumza kwa muda mrefu; na wote walisema; wakieleza sababu zao za kudai Serikali ya Tanganyika. Nilisisitiza kwao kwamba zote zilikuwa ni sababu za kuwataka wawadhibiti viongozi wetu na kuwataka watuongoze kwa kufuata sheria na Katiba ya Nchi yetu. Hapakuwa na sababu hata moja ya kuwafanya wadai Serikali ya Tanganyika, maana hata ukiwa na Serikali ya Tanganyika bado viongozi wetu wanaweza kukiuka sheria na Katiba ya Nchi na dawa haitakuwa ni kuigawa nchi tena na kuongeza serikali bali ni kuwadhibiti viongozi wahalifu. Baadaye hoja hizi nilizirudia bungeni.
[/TD]
[TD]18
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kilikuwa kikao kirefu na kigumu. Sina kawaida ya kulizwa na mambo ya siasa lakini katika kikao hiki nilishindwa kujizuia kulia. Sikupata maelezo ya maana ya kuwafanya watu wafanye walivyofanya. Nilipouliza kwa nini hawakupinga hoja ya Serikali tatu kama tulivyokuwa tumekubaliana majibu ya viongozi wetu wakuu yalikuwa ni ya ajabu kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa wakali kama mbogo! Tena walikuwa wakiwatukana wenzao (yaani wabunge wa Zanzibar) kwa kuwataja majina.
[/TD]
[TD]27
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Katika suala la Utanganyika, inaelekea kuwa Rais si miongoni mwa marubani, yeye anakokotwa tu, moyo wake haumo.
[/TD]
[TD]51
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kosa kubwa la Rais (na ni kosa kubwa), ni kule kukubali kushirikishwa kosa, badala ya kuwafukuza wale waliomshauri ashiriki kosa lao. Waziri Mkuu aliposhindwa kupinga hoja ya Utanganyika alipaswa kujiuzulu; lakini aliposhindwa kufanya hivyo, na badala yake akamshauri Rais naye akubali kuwa geugeu, Rais angemfukuza pale pale na kuteua Waziri Mkuu mwingine. Rais hakufanya hivyo; na badala yake Rais naye akakubali kweli kuwa geugeu na kushiriki kosa la washauri wake.
[/TD]
[TD]53
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole, lakini ni kiongozi dhaifu; au upole wake na udhaifu wake --------- na watu ambao wala si wema wala wapole kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu, Kipindi chake cha pili kinakaribia kwisha, kwa Taifa letu jambo muhimu zaidi kwa sasa ni uongozi wa Chama na Serikali, na ni nani atakayechukua nafasi ya Rais baada ya Uchaguzi Mkuu mwakani,
[/TD]
[TD]59
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kitu kimoja ambacho hatuwezi kutazamia ni kwamba siku moja Nchi Moja hii itakuwa nchi mbili, kwa uongozi wa CCM.
[/TD]
[TD]66
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CHAMA CHA MAPINDUZI kitakapobadili sera yake ya Muungano wa Serikali Mbili, sera yakempya itakuwa sera Muungano wa Serikali moja. Chama Cha Mapinduzi chenye wanachama wenye akili, na ukweli, na ujasiri, hakiwezi katu kukubali sera ya serikali tatu, kikijua wazi wazi kwamba matokeo na shabaha ya sera hiyo ni kuiua, na kuizika Tanzania. Chama Cha Mapinduzi kikiwa na msimamo huo na wala kisiuonee haya, Tanzania itadumu.
[/TD]
[TD]68
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
tatizo la Mwinyi Ni Kukubali Kushirikishwa Kwenye Kosa Na Tatizo La Jk Ni Kukubali Mabadiliko Ya Katiba Ya Zanzibar Chini Ya Kinachoitwa Muafaka
 
So long as wazanzibari wata demand utambulishi wa taifa lao na ni haki yao ya msingi swala la serikali moja aliewezekaniki, serikali tatu kwa mujibu wa jaji warioba ni kuuvunja muungano maana huko mbele hakuna mtu atakae taka kuona kama kila mtu ana mamlaka kamili why should we bother with matters that could be handled under EAC.

Ni kupoteza pesa tu, vilevile itakuwa ngumu sana wabara kukubali raisi wa jamhuri kutoka ZnZ, likewise W-ZnZ wata demand zamu ya uraisi we might as well take whats ours, yaani tujenge bunge tutoe na wabunge kwenda kujadili mambo machache kwa faida ya mataifa mawili, hapo hapo tunabunge la EAC na ndio kwanza changa in the future you know gharama zitaongezeka na majukumu mengi yataamia mule, sasa kunafaida gani ya kubaki na tanzania kwa mtindo wa mapendekezo ya warioba.

Nikiri baada ya kumsikiliza mzee warioba inaonekana kuna matatizo lakini mengi yanahitaji elimu zaidi kuliko kuziita kero za muungano. Kuna kutouelewa maana ya national devolution kwa upande wa bara especially ZnZ kutaka kufanya vitu kama taifa pia kuna kutokufahamu maana ya serikali kuu ambapo ZnZ lazima imezwe katika utaifa wa Tanzania kuna mkanganyo wa mambo mengi hapo, lakini vingi katika vilivyo orodheshwa kama kero haviwezi kupatiwa majawabu ya kipekee kama tunataka kubaki na Tanzania maana ya kuungana inabidi huweze ku-compromise (si hata watu wawili wanapofunga ndoa lazima kuwe na compromise ya lifestyle ili waishi kwa amani pamoja).

Mfumo wa sasa ndio njia sahihi ili wa-znz waweze fanya mambo kadhaa kwa namna zao ambayo si ya muungano. Lakini tukianza kukagua na kuangalia habari za makatibu wakuu wametoka wapi na mambo mengine tosh ujue huko si kutafuta suluhisho bali tayari kumeshakuwa na sisi na wao kwa uelewa wangu mdogo tukishafika hapo na kila mtu kasimama on that ground hakuna sababu tena ya kuwa pamoja.
 
Maelezo matamu sana lakini umma ndio wenye kuchagua aina ya muungano wanaotaka sio watu wachache walazimishe walio wengi kufuata mtazamo wao hapo tutakuwa tumeisigina demokrasia hofu iko wapi wacha watanganyika na wazanzibar wachague kile wanachokitaka
 
Back
Top Bottom