Serikali 2: Hoja ya CCM ingekuwa hii!!!!

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Badala ya CCM kutaka serikali 2 wangetumia wingi, nguvu, umaarufu na uhodari wao katika kukemea Zanzibar warudishe vidole vyao kwenye mstari. Wazanzibar wakemewe wasifunje katiba ya Muungano na wapewe adhabu kali kwa kitendo hicho kwani waazilishi wa chokochoko za kuchezea katiba ya muungano wanafahamika kwa majina yao hata nyumba zao kwanini CCM na serikali zake zinalegalega katika kuilinda katiba? Miungano yote duniani huwa inalindwa kwa kutumia sheria, nguvu, hila, vitisho na hata ilibidi umwagaji damu. Hivi nani kakwambia majimbo yote ya Marekani yanaridhika na muungano wao uliofanywa zaidi ya miaka 200 iliyopita na akina Washington? Nani kasema muungano wa visiwa vya Uingereza hauna matatizo? nani kamwambia muungano wa Ulaya hakuna nchi wanachama wasio na manung'uniko? Kinachoilinda miungano yote duniani ni kulinda na kutekeleza makubaliano ya muungano kwa uwaminifu, sheria kali saaaana kwa wanaotaka kuuvunja na wananchi wa pande zote kuendelea kuziona faida za muungano kwa uwazi.
Badala ya CCM kufanya mchezo wa kuigiza wa kutaka muungano wa serkali mbili bila kuonyesha kukerwa na uvunjifu wa katiba unaofanywa Zanzibar ni kuwaonea Watanganyika na hawataweza kuwazuia kudai Tanganyika yao pia kwa gharama yoyote.
 
Subutu wana ubavu wa kukemea Zenji. Chezea Zenji wewe.
 
Ukishindwa kujenga hoja si unabaki kusema sisi wengi, oh mara hawa hawautakii mema muungano na mambo mengine kibao. Uwezo wa kuwakemea Wazenji hawana kwa kuwa wanajua wakiwaudhi watatangaza kujitenga.
 
CCM wanawakejeli watanganyika maana wengi hawajui haki zao.
 

Well Said!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…