Serikali 3 / Majimbo

Serikali 3 / Majimbo

JOASH MUSSA

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
515
Reaction score
199
Wana JF,

Nchi yetu inaenda kufanya mabadiliko ya katiba, na kwa sasa baada ya tume ya Jaji Warioba kutoa rasimu ya pili ya Katiba na yatokanayo inatupasa kuendelea kuumiza kichwa kwa kujaribu kutoa michango hasa juu ya muundo wa Serikali ili kudumisha Muungano wetu na kufuta 'Kero za Muungano',

Nilipata kusikia Wazanzibari wakisema hawakotayari kuchangia sawa na Tanganyika gharama za kuendesha Serikali ya Muungano, na ni kweli hawataweza! Hivyo gharama zote zitabaki kwa Tanganyika.

Ni rahisi kwa Tanganyika nao kukwepa gharama, na kuiacha Serikali ya Muungano solemba hivyo kuvunjika kwa muungano wenyewe

Ila, Chadema wana Sera nzuri inayoweza kufuta kero zote za Muungano kwa kuweka serikali za Majimbo, kuna nchi nyingi duniani zimeungana kwa namna hii na zimekuwa na nguvu kubwa, hakuna kero na tena kwa miaka mingi

Mfano mkuu ni United States Of America, na hata Kenya juzi walipobadili katiba yao wameingiza system za Majimbo

Majimbo yatachangia Maendeleo kwa haraka kwa wananchi na pia yatachangia gharama za uendeshaji wa serikali kuu.... Ambapo kutakuwa na Serikali moja yenye rais au Waziri Mkuu na Mawaziri wachache maana shughuli nyingi za kiuchumi zitakuwa chini ya Majimbo ambayo hayatazidi 7 au kama itakavyoamuliwa

Ni mawazo tu..
 
Back
Top Bottom