Msemaji wa serikali Bwana Msingwa leo ametoa taarifa kwa umma kwamba hadi kufikia jana tarehe 11.9.2021 tayari watanzania 345,000 wamepata chanjo ya Covid 19.
Bwana Msigwa ameongea kua kutokana na muitikio mkubwa wa watu kutaka chanjo, sasa mpango uliopo ni kusambaza zaidi chanjo kwenda vijijini ili watu wasifuate chanjo mbali na makazi yao.
Kwa mtazamo wangu, kwenye hili la chanjo serikali imechemka big time, leo karibia miezi 2 ama wiki 6 toka chanjo izinduliwe na Rais watu 345,000 tu ndio waliochanjwa. Kwa hesabu ni kwamba watu 57,000 ndio wanachanjwa kwa wiki sawa na watu 8,124 kwa siku.
Tukienda na hizi takwimu, chanjo 1,008,400 za J&J tulizoletewa na Marekani itachukua siku 124 ama miezi 4 kuzimaliza. Kumbuka tuna chanjo za msaada kama hizo milioni 11 za Covax zitaletwa, hizo zitahitaji zaidi ya miaka 4 kuisha kama tukiendelea na spidi hii. Tukumbuke pia kua chanjo toka imetengenezwa inakaa miezi 6 ndio inaisha muda wake ama ku-expire. Hatujajua hizi tulizoletewa zina muda gani toka zitengenezwe.
Na wataalamu wanasema ili ufikie herd immunity unatakiwa angalau uchanje 70% ya population yako, kwa Tanzania tunatakiwa kuchanja watu milioni 42 angalau. Kwa hapo tutahitaji miaka si chini ya 15 kumaliza kuchanjwa kwa spidi hii.
Hilo halitoshi bado tukimaliza kuchanjwa watu milioni 42, tutatakiwa kuanza kuwachanja tena booster ama baada ya miezi 6 toka tumeanza kuchanjwa tunatakiwa kuanza kuchanja booster, yaani chanjo mpya na booster ziende simultaneously.
Serikali kabla haiajaanza kununua chanjo nyingine kutoka kwenye mkopo iliochukua wa zaidi ya Trilioni moja, ifanye analysis ya uhakika, tusije kununua chanjo zika expire bila kutumiwa na halafu tukaachwa na deni kubwa la kulipa huku hela imeenda bure.