Serikali anzisheni kampeni maalum ya kilimo cha mazao ya Mafuta

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
20,419
Reaction score
39,217
Wasalaam,

Naomba kutoa wito kwa serikali hususani wizara ya kilimo chini ya Mheshimiwa Bashe kuanza mkakati kabambe wa kuwekeza kwenye kilimo cha mazao ya mafuta kama alizeti, karanga, ufuta, michikichi n.k

Kwa hali iliyopo ambapo nchi uzalishaji wa mafuta ya kula ni 45% na tunaagiza 55% bado na inapaswa tujihurumie na tutambue tumefanya kosa kubwa sana. Kwa ardhi kubwa yenye rutuba kuagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi ni tusi kwa nchi yetu.

Natoa wito kwa wizara ya kilimo na taasisi zake sasa kuanza kampeni kabambe ndani ya miaka mi5 kuhakikisha nchi sasa inawekeza nguvu zaidi katika kilimo cha mfuta ya kupikia ili tuweze kujitosheleza kwa mahitaji ya ndani na pia kuweza kuanza kuuza mafuta nje ya nchi.

Hakuna linaloshindikana kama mkiweka siasa pembeni na kufanya kwa weredi na mtaalamu ili kufikia lengo maana ardhi tunayo, nguvu kazi tunayo, wataalamu tunao, pembejeo zipo ingawa hapa zinabidi zipatikane kwa urahisi.

Kila la kheri mumsaidie rais na wananchi acheki kujificha kwenye kichaka cha vita ya urusi na Ukraine au Covid19 kila mara mambo yanapo enda kombo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huku kwetu Kyela halmashauri inatoa miche ya michikichi ya kisasa BURE. Wanachokitaka uwaoneshe shamba lililoandaliwa kwa ajili ya kilimo husika tu.

Program ya miche ya kisasa pia ipo Kigoma, chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Nawe ukiihitaji wasiliana na afisa kilimo wa Halamashauri yako.

Pia serikali inao mpango wa kilimo cha Halizeti mkoa wa Singida. Nadhani lengo ni kuendeleza pia kwa mikoa ya Dodoma na Manyara.

Tatizo sio kuanzisha kampeni, tatizo ni mindset zetu, tatizo ni kuendeleza program zinazoanzishwa. Watumishi wanatamani kupiga hela tu, na wananchi tunapenda kulaumu...
 
Hivi kilimo cha bio diesel bongo kimeishia wapi

Ova
 
Unahitajika mpango serious. lakini serikali hii mpango gani imewahi fanya ukafanikiwa vizuri.
 
Upo sahihi....hiyo ni njia ya kudumu ya kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula nchini.
 
Wasalaam,

Naomba kutoa wito kwa serikali hususani wizara ya kilimo chini ya Mheshimiwa Bashe kuanza mkakati kabambe wa kuwekeza kwenye kilimo cha mazao ya mafuta kama alizeti, karanga, ufuta, michikichi n.k

Kwa hali iliyopo ambapo nchi uzalishaji wa mafuta ya kula ni 45% na tunaagiza 55% bado na inapaswa tujihurumie na tutambue tumefanya kosa kubwa sana. Kwa ardhi kubwa yenye rutuba kuagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi ni tusi kwa nchi yetu.

Natoa wito kwa wizara ya kilimo na taasisi zake sasa kuanza kampeni kabambe ndani ya miaka mi5 kuhakikisha nchi sasa inawekeza nguvu zaidi katika kilimo cha mfuta ya kupikia ili tuweze kujitosheleza kwa mahitaji ya ndani na pia kuweza kuanza kuuza mafuta nje ya nchi.

Hakuna linaloshindikana kama mkiweka siasa pembeni na kufanya kwa weredi na mtaalamu ili kufikia lengo maana ardhi tunayo, nguvu kazi tunayo, wataalamu tunao, pembejeo zipo ingawa hapa zinabidi zipatikane kwa urahisi.

Kila la kheri mumsaidie rais na wananchi acheki kujificha kwenye kichaka cha vita ya urusi na Ukraine au Covid19 kila mara mambo yanapo enda kombo.

#MaendeleoHayanaChama
Wazo zuri sanaaa Ila sio Kwa serilikali kama hii

Ngoja tuone Waziri Bashe ataishia wapi maana ana mawazo mazuri
 
Wasalaam,

Naomba kutoa wito kwa serikali hususani wizara ya kilimo chini ya Mheshimiwa Bashe kuanza mkakati kabambe wa kuwekeza kwenye kilimo cha mazao ya mafuta kama alizeti, karanga, ufuta, michikichi n.k

Kwa hali iliyopo ambapo nchi uzalishaji wa mafuta ya kula ni 45% na tunaagiza 55% bado na inapaswa tujihurumie na tutambue tumefanya kosa kubwa sana. Kwa ardhi kubwa yenye rutuba kuagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi ni tusi kwa nchi yetu.

Natoa wito kwa wizara ya kilimo na taasisi zake sasa kuanza kampeni kabambe ndani ya miaka mi5 kuhakikisha nchi sasa inawekeza nguvu zaidi katika kilimo cha mfuta ya kupikia ili tuweze kujitosheleza kwa mahitaji ya ndani na pia kuweza kuanza kuuza mafuta nje ya nchi.

Hakuna linaloshindikana kama mkiweka siasa pembeni na kufanya kwa weredi na mtaalamu ili kufikia lengo maana ardhi tunayo, nguvu kazi tunayo, wataalamu tunao, pembejeo zipo ingawa hapa zinabidi zipatikane kwa urahisi.

Kila la kheri mumsaidie rais na wananchi acheki kujificha kwenye kichaka cha vita ya urusi na Ukraine au Covid19 kila mara mambo yanapo enda kombo.

#MaendeleoHayanaChama
Changamoto kubwa tulio nayo katika nchi za Afrika ni kuwaingiza madarakani ambao ni wafanyabiashara na waendekeza njaa na makundi.Miradi mingi inaishia isikojulikana pamoja na mbwembwe wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo.Nchi za Afrika zinapoteza pesa nyingi kwa kuuza mazao ghafi nje ya nchi.
 
Changamoto kubwa tulio nayo katika nchi za Afrika ni kuwaingiza madarakani ambao ni wafanyabiashara na waendekeza njaa naakundi.Miradi mingi inaishia isikojulikana pamoja na mbwembwe wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo.Nchi za Afrika zinapoteza pesa nyingi kwa kuuza mazao ghafi nje ya nchi.
Tena wengi hata si wafanyabiashara bali madalali wa wawekezaji wanyonyaj na wapiga dili! Ndo mana inabid tuwe na sera ya kitaifa ili tusitembelee tu ilan za chama kinachoshinda.
Pia nafikiria uboreshaj wa uzalishaji wa mahitaji muhim kwa viwanda vidogo vidogo ngaz ya familia. Mf ni ukamuaj wa alizet na kujitengenezea sukar.
Ni heri serkali ipate kodi kidogo ya viwanda vikubwa vya ndan lakin isihitaji kununua pesa za kigen nyingi kwa ajiri ya import!
Haya yote hayawezekani bila KUNANILII...!
 
Kuna vichekesho sana nchi hii. Zamani kulikuwa na mafuta ya pamba sijui yameishia wapi? Ilitakiwa sehemu kama Mtwara walime karanga na Ufuta tupate mafuta. Wasukuma na wamasai wangetoa Samli. Singida na Dodoma na manyara yote wangejikita kwenye Alizeti na Karanga. Lakini watu wapo busy na kutanua tu.
 
Back
Top Bottom