#COVID19 Serikali bado ina nafasi ya kushawishi Watanzania chanjo ya Corona

#COVID19 Serikali bado ina nafasi ya kushawishi Watanzania chanjo ya Corona

MKILINDI

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
791
Reaction score
1,120
Kwa muelekeo wa ugawaji na uchanjaji wa chanjo ya UVIKO19 Tanzania na malumbano kati ya viongozi wa serikali wenyewe kwa wenyewe kuhusu kuchanja Corona yaonekana wazi kuwa serikali yaweza kushindwa vita hii, kwa kuwa, kwanza ni hiari lakini pia ilishajikwaa mwanzoni kuhusu chanjo hiyo kwa awamu iliyopita na utandawazi haumfichi mtu. watanzania wana kumbukumbu za video za viongozi waliokuwa wakihudumu na misimamo yao kuhusu chanjo kwa Serikali iliyopita.

Rais Samia Suluhu, alikuwa sahihi kuwateua mawaziri wa wizara hii kwa wakati ule ikiwa tu angeendeleza msimamo, imani, na mitizamo ya mtangulizi wake katika suala la ugonjwa huu wa Corona lakini kwa kuwa amegeukia katika duru zingine hivy kwa sasa hayupo sahihi kwa kuwarudisha walewale kwakuwa anachokiamini si kile walichokuwa wanakiamini aliowateua katika wizara husiika kwa kipindi chake na hiki ni mojawapo ya kitu kinacholea ugumu wa zoezi.

Bado serikali ya TANZANIA ina nafasi ya kuwashawishi watanzaania kuhusu chanjo kwa kufanya haya.

1) Wizara husika na viongozi wa wizara husika wabadilishwe. ili viongozi wapya wajao waweze kueleweka kwa watanzania pindi wanapotoka kuwaeleza watanzania kuhusu chanjo ya Corona. Leta sura mpya za wizara ya afya ambazo hazikuwa na misimamo ya mitishamba kama hawa waliopo.

2) Serikali ikubali kuwa mwanzoni ilikosea na iwaelekeze watanzania kuwa tubadili muelekeo na twende na muelekeo huu.

3) Imteue Waziri wa Afya mwenye skills za uongozi si lazima awe na proffessional yake ya afya. skills za uongozi zinatosha kufanya vizuri kwenye seniority position hata kama huna prosessionalism. tumkumbuke jk hapa aliwahi kusema "hakuna chuo cha kusomea uwaziri"

4) Serikali itangaze takwimu ya wagonjwa wa covid hata kwa data za kupika ili kugusa intimancy ya mtu na kuona umuhimu wa kuchanja.
 
4. Kwamba wapike data huu nao ushauri?

Hujiulizi wananchi wa kawaida hawana habari na hiyo Corona,pamoja na kuwa ipo?

Ni viongozi tu wanalazimisha waiogope ila wananchi maisha yanaendelea Kama kawaida

Ungewashauri wabadili approach waseme huu ukweli kuwa wananchi wanaopona baada kuugua Corona ni wengi na wametibiwa kwa dawa gani.

Kuliko kulazimisha hofu,eti usicheze na Corona, utafikiri kila anayeugua lazima afe.
 
4. Kwamba wapike data huu nao ushauri?
Hujiulizi wananchi wa kawaida hawana habari na hiyo Corona,pamoja na kuwa ipo?
Ni viongozi tu wanalazimisha waiogope ila wananchi maisha yanaendelea Kama kawaida...
YAP ni ushauri. tena ushauri wa ndani. kwa kipindi hiki watanzania wengi wanasikiliza vyomba vya habari na wanasikilizia nini kinaendelea kwenye ugonjwa huu.

ikiwa unataka jambo lako liende kama unavyotaka tengeneza hofu. kwa sasa kumepoa kwakuwa hata idadi ya wagonjwa hausikii mtu anachukulia poa hata tahadhari zimepungua dhidi ya huu ugonjwa.

ukisikia idadi ya wanaogua wamefika laki8 dar es salaama pekee hyo inajengeka hakuna atakayetaka kuverify kam akweli kuna wagonjwa laki8.
 
Sasa unamtuma Steve Nyerere ashauri watu, wakati yeye mwenyewe hajitambui, mtu gani asiyeekwa atachukulia hii issue serious? Kuna mambo ya msingi ya kuelimishana kuhusu chanjo. Na lazima yafanywe na watalaamu. Bongo movie hawawezi kuongoza uhamasishaji. Bora hata Bongo Fleva
 
Bahati mbaya tusitafute wachawi serikali imejitahidi mtatizo ni watanzania kupenda uongo na wengine ni mambumbumbu huo ndio ukweli. wanaofiwa na ndugu wanajua umuhimu wa chanjo.
 
YAP ni ushauri. tena ushauri wa ndani. kwa kipindi hiki watanzania wengi wanasikiliza vyomba vya habari na wanasikilizia nini kinaendelea kwenye ugonjwa huu. ikiwa unataka jambo lako liende kama unavyotaka tengeneza hof..
Unataka wenye misaada yao wawaambie lockdown Ili watoe zaidi mikopo kisingizio maambukizi yapo juu?

Hilo wapo macho ukifanya lockdown utaua wengi kwa njaa kuliko Corona, nafuu hivyi wanavyofanya hii comedy.
 
Back
Top Bottom