Serikali binafsisheni TANESCO sio Bandari

Serikali binafsisheni TANESCO sio Bandari

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,588
Reaction score
22,752
Umeme,maji na internet ni nyezo zinazofanya vijana wengi wajiajiri na sector binafsi zikue.

Cha ajabu mnaenda kubinafsisha Bandari ambayo raia wa kawaida haelewi atanufaikaje na ubinafsishaji huo.

Raia tusio na upeo tunajiunga kupinga ubinfsishaji wa bandari yetu hata kama huo mkataba hatujausoma kwa sababu hatuelewi kivip bandari yetu haina ufanisi huku Bandari yetu inaongoza kwa kodi kubwa ya kuingiza mizigo hapa nchini na ukanda wa SADC.

Raia huku mtaani tunashangazwa kivip bandari yetu ipelekwe mikononi mwa wawekezaji kwa mkataba ambao mbovu huku mmemfukuza ELON MUSK kuwekeza kwenye internet ya kasi kwa sababu za kizee na zilizopitwa na wakati.

Vijana wengi tumeajiajiri kupitia nyenzo za internet, maji na UMEME.

Nakumbuka enzi za Jakaya Kikwete tuliambiwa gesi ya Mtwara inaenda kusolve tatizo la umeme na tutauza hadi nchi za nje sijui kikatokea nini mpaka mnaona aibu kuzungumzia gesi ya Mtwara.

Ni juzi tu tumetoka kwenye msimu wa mvua leo tumeshaanza mgao wa umeme.

Kama mnataka Watanzania tuwakubari binafsisheni vitu ambavyo vitamgusa direct mtanzania hayo ya bandari na kupelekana dubai tunaisi ni michongo yenu binafsi ya kuila nchi.

SIASA HAPA NCHINI IMEKUWA NDIYO BIASHARA KUBWA KULIKO BIASHARA ZOTE NDIYO MAANA VIONGOZI WANARITHISHA MADARAKA KWA WATOTO NA VIZAZI VYAO NA NDIYO MAANA CCM HAITAKI KUTOKA MADARAKANI.

Kingine raia tunataka tubadilishe utawala sio kama tunaakini Vyama pinzani vina wazalendo lahasha tunataka tubadilishe baadhi za koo nazo zionje utamu wa nchi kwa sababu tunapoenda kuna koo hazitakuja kuona tumaini kwa sababu kwenye koo nzima hakuna kiongozi hata wa kijiji na hii ina boost povert chain.
 
Ukatikaji wa UMEME unatuongezea umasikini huku mtaani.
 
Umefikilia mbali mkuu ikiwezekana ata TRC maana ilishajifia zake Toka zamani
 
Umefikilia mbali mkuu ikiwezekana ata TRC maana ilishajifia zake Toka zamani
Wanakomalia bandari ambayo sisi huku chini hatutaziona hela zake kutoka kwa hao DP world
 
Km serkali haina uwezo wa kuongoza iondoke waingie wenye uwezo sio kubinafisisha tanesco au bandari tena kwa mafisadi ya kiarabu
 
Km serkali haina uwezo wa kuongoza iondoke waingie wenye uwezo sio kubinafisisha tanesco au bandari tena kwa mafisadi ya kiarabu
Umeme angalau tutaangaziwa tutampima muwekezaji vizuri.
 
Nipo hapa kijiweni kwangu napiga soga umeme hamna!
Sioni ubaya akatafutwa muwekezaji mbia mwenye uzowefu kutoka Uingereza, Marekani aidha kanada, akaja hapa Tanzania na majawabu yatakayo tuondoshea kukatika katika kwa umeme, kwa hali kufikia malengo kwa taifa hili itayafikia kwa tabu sana.
-Nisiulizwe kwa nini sikutaja waarabu, ukisikia dubai jua huyo ni mmarekani, Saudi Arabia, huyo ni mmarekani, tusipige chenga tukaenda kwa madalali, tuwafuate wahusika.
 
Hii TANESCO ndiyo DPW wangepewa mkataba hata wa milele ingependeza sana tupate umeme wa uhakika masaa yote kuliko wapewe bandari.
 
Tanesco.. ibinafsishwe part ipi ?

Kubinafsisha upande wa mitambo ya uzalishaji ni hatari sanaa..

Waruhusu wawekezaji tofauti.. katika Tanesco.. wenye Technolojia tofauti tofauti..
 
Back
Top Bottom