Serikali: EWURA inafanya tathmini ili kupata bei moja ya Diesel na Petrol nchi nzima

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 2, leo Aprili 3, 2024 Jijini Dodoma.

Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha ameuliza "serikali ina mpango gani ili bei ya petroli na dizeli iwe moja Nchi nzima?"

Naibu Waziri Judith Kapinga amejibu "Serikali kupitia Ewura inafanya tathimini kufanya bei ya petroli na dizeli nchi nzima, mfumo huo uliokuwa unatumika miaka ya nyuma ulikwama kwa changamoto zikiwemo za kisera na kiusimamizi hivyo wafanya biashara wa mafuta walipanga bei zao kuendana na ushindani wa soko, tathimini ikiweza kukamilika Serikali itafanya utekelezaji bila kukutana nachangamoto za awali za kiusimamizi."

Geofrey Mwambe Mbunge wa Masasi Mjini ameuliza Je, Lini Serikali itakamilisha usanifu wa mradi wa maji mto rufiji litokalo Bwawa Nyerere kutumika mikoa ya Lindi na Mtwara?"

Jumaa Aweso, waziri wa Maji amejibu kuwa Serikali inaendelea na tathmini ya awali wa mradi wa maji mto rufiji litokalo Bwawa Nyerere kupeleka maji mikoa ya Lindi na Mtwara kuhakikisha maji kupatikana katika mikoa hio, inaendelea na mapitio ya usanifu wa mradi huo kuhakikisha maji kupatikana kwa maji pembezoni ambapo bomba kuu litakuwa limepita.
 
Naibu waziri wa Nishati mh Kapinga amesema EWURA inafanya tathmini Ili Kupata Bei Moja ya Diesel na Petrol Nchi nzima

Kapinga alikuwa akijibu swali la mbunge wa Arusha mh Mrisho

Source: Mwananchi
 
Rubbish answers from rabid minds
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 2, leo Aprili 3, 2024 Jijini Dodoma.

Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha ameuliza "serikali ina mpango gani ili bei ya petroli na dizeli iwe moja Nchi nzima?"

Naibu Waziri Judith Kapinga amejibu "Serikali kupitia Ewura inafanya tathimini kufanya bei ya petroli na dizeli nchi nzima, mfumo huo uliokuwa unatumika miaka ya nyuma ulikwama kwa changamoto zikiwemo za kisera na kiusimamizi hivyo wafanya biashara wa mafuta walipanga bei zao kuendana na ushindani wa soko, tathimini ikiweza kukamilika Serikali itafanya utekelezaji bila kukutana nachangamoto za awali za kiusimamizi."

Geofrey Mwambe Mbunge wa Masasi Mjini ameuliza Je, Lini Serikali itakamilisha usanifu wa mradi wa maji mto rufiji litokalo Bwawa Nyerere kutumika mikoa ya Lindi na Mtwara?"

Jumaa Aweso, waziri wa Maji amejibu kuwa Serikali inaendelea na tathmini ya awali wa mradi wa maji mto rufiji litokalo Bwawa Nyerere kupeleka maji mikoa ya Lindi na Mtwara kuhakikisha maji kupatikana katika mikoa hio, inaendelea na mapitio ya usanifu wa mradi huo kuhakikisha maji kupatikana kwa maji pembezoni ambapo bomba kuu litakuwa limepita.

Tofauti ya bei iko wazi na huhitaji kuwa waziri kulijua hilo. Tatizo ni uongo wa kila siku wa hawa ndugu zetu. Tofauti ya bei kati ya mkoa na mkoa inatokana na gharama za usafirishaji tu basi.
 
Tanzania hakuna bunge. Kuna kikao cha ccm.
Ni wajinga tu wanaweza kuamini maneno ya mbunge aliyeuliza swali na majibu ya naibu waziri aliyejibu hilo swali. Huyo naibu waziri hatakiwi kuwa anakikalia hicho kiti kwa sasa.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom