Serikali fanyeni haya ili tutoe ushindani AFCON 2027

Serikali fanyeni haya ili tutoe ushindani AFCON 2027

Mtemi Mbojo

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
891
Reaction score
1,569
Nikiwa kama mdau wa michezo hasa Mipira wa Miguu, nashauri Serikali kufanya haya ili kuboresha kiwango cha mpira nchini, na hata ushiriki wetu kwenye mashindano yajayo ya AFCON,2027 yatakayo fanyika nchini kwa kushirikiana na wenzetu wa Kenya na Uganda.

1. Tutafute Kocha wa daraja la juu wa soka ambaye analifahamu soka la Africa na dunia kwa ujumla. Yule ambaye rekodi yake haina shaka yoyote.Nampendekeza kocha wa zamani wa Zambia na Ivory Coast ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Ufaransa , Herve Renard ,tukishindwa huyo twende na kocha wa zamani wa Aly Ahly ya Egypt/Mamelody Pitso Mosimane au Mkongo Florent Ibenge, bila kusahau suala la timu kukaa kambini muda mrefu,miezi 6 itapendeza zaidi

2. Kwa maendeleo ya muda mrefu tuchukue makocha hata 10 vijana na wale wa makamo wapelekwe nchi za Ulaya hasa Ujerumani, kwa mafunzo ya soka {Burundi walishafanya hili)..napendekeza makocha wafuatao wapate hiyo fursa,

i. Zuberi Katwila, Selemani Mtola, Minziro, Mecky Mexime, Mbwana Makata, Edward Augustino, Pawasa, huyo kocha wa sasa Prison, Julio, na wengine kadiri Serikali itakavyoona inafaa ila kwa kuanzia tunaweza tupeleke Makocha 10, na wakirudi wapewe timu za taifa na hata vilabu kwa malengo maalumu.
Kuhusu gharama tunaweza OMBA ufadhili kwa wenzetu wa Ujerumani

3.Tuboreshe chuo cha Michezo cha Malya Mwanza,na hawa watakaopelekwa Ujerumani wanaweza kuwa Wakufunzi hata wa muda kule chuo cha Michezo Malya,

TUKIYAFANYA HAYA NINAAMINI KIWANGO CHA MPIRA NCHINI TANZANIA KITAPANDA
 
Yule jamaa hatuwezi kumtoa pale alipo kwa Sasa yani ni haiwezekani
Hayo ya program ni sawa yakifanyika itakuwa poa

Sema labda kingine tujitahidi wale tunaohitaji kuwa tumia Afcon waingie Simba yanga na Azam na kuanza kupata uzoefu wa mechi za ushindani kimataifa
 
Nakuelewa Kiongozi..ila timu ya Wanawake ni kama ameshushwa daraja hivi..ila tungejaribu..tukishindwa hata huyo wa Zambia wa sasa atatufaa..tunawapora tu..money talks
 
Nakuelewa Kiongozi..ila timu ya Wanawake ni kama ameshushwa daraja hivi..ila tungejaribu..tukishindwa hata huyo wa Zambia wa sasa atatufaa..tunawapora tu..money talks
Money talks kwa nchi inayoamini kwenye michezo kumbuka yule hataki ten percent ye ni ana standard zake yani ni haiwezekani trust me
 
Back
Top Bottom