Nashangazwa na serikali hasa ukizingatia wameweka wasomi wengi sana. Kwasababu ya mazoea wasomi wetu sio wabunifu na hakuna sera siku hizi na mapingo mizuri zaidi ya kumsubiria Magufuli anasema nini.
1. Elimu: Kwanini tunakurupuka sasa na kujenga vibanda tunavyoita madarasa! wakati kuna kitengo cha takwimu ambacho kinatakiwa kujua Tanzania tuna watoto wangapi kila kijiji! na isitoshe watoto wanaanza darasa la kwanza na miaka 7 sasa inakuwaje serikali inashitukizwa kwa idadi ya watoto wa shule. Badala ya kusifia kila kitu tujiulize maana kuna watu hawafanyi kazi yao au hakuna mipangilio ambayo inafuata takwimu ambazo ni muhimu sana kwa mipango
2. Afya kwenye Afya serikali inajenga hospitali kila wilaya lakini wanajenga kwa mazoea na amri sio kwa kufuata takwimu wilaya ya mkoa wa shinyanga huwezi kulinganisha na wilaya mkoa wa rukwa kwa idadi ya watu lakini cha ajabu ni copy na paste kama vile kila wilaya au mkoa ni sawa. Hospitali na clinic zinatakiwa kujegwa kutokana na takwimu za sehemu na sio kutokana na wilaya za kisiasa. Hivyo washauri wangetakiwa kuwa na data na kumuonyesha Magufuli umuhimu wa hili badala yake wameweka nazoea na kazi yao ni kugombeza kwenye kamera ili waonekane. Sasa ugombezaji unahitaji PHD?
3. Mfano mwingine wa Afya tunaiga mfumo wa hospitali wa ulaya wakati wenzetu wana nchi ndogo na wako karibu karibu ni kwanini kusiwe na mpangilio wa kuwa na magari yenye madoktari tofauti kupita vijijini kutoa chanjo watu walipo, kutoa huduma za macho, meno na vyakula. Magojwa yenye gharama kubwa yanasababishwa na kisukari na pressure sasa haya magojwa yanahitaji elimu maana ukitoa elimu utapunguza wagojwa sasa kwanini hakuna mfumo wa kinga tuna mfumo wa matibabu tu na ndiyo maana watu hawaishi miaka mingi kama nchi za Cuba mfano.
4. Elimu: Badala ya kupeleka vijana JKT kula kulala ni kwanini vijana waliopewa mkopo na serikali wana vyuo wasiwe na mwaka mmoja wa kutoa huduma kwa jamii kama kufundisha na serikali kutoa punguzo la madeni yao. Hii ingesadia vijana sana hata kama wangelipwa kidogo badala ya vijana wasomi kukimbia mchaka mchaka. Vita ya sasa sio ya bunduki ni ya teknologia na teknologia inahitaji elimu.
Kuna mengi lakini serikali iweke utamaduni wa kutumia data kwa mipangilio hili la madarasa linaonyesha hakuna mpangilio.