Tetesi: Serikali fanyeni tafiti kwenye samaki na mazao ya shamba ongezeko la wagonjwa wa saratani(cancer) kanda ya ziwa

ni kweli kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa kansa hasa Bunda ni vema serikali ifanye utafiti kwani kinga ni bora kuliko tiba

Inaelekea kuna katatizo kakubwa huko kanda ya ziwa kanakohusu Cancer, lakini pia kama waliwahi kukana kuwa wanakula mapanki ya samaki iliyoonyeshwa ndani ya "Darwins Nightmare" kwanini matokeo hayo tuyategemee ktk mustakabali wa Cancer study inayoombwa hapa?
 
Na isiwe mwanza tu, maana lile ziwa ni kubwa na linahusisha mikoa kadhaa. KAMA UNAHISI TU SAWA HAKUNA TATIZO,ILA KAMA NI KWELI KUNA HAYO MAMBO HAKIKA HATA SOKO LA HAO SAMAKI LITAATHIRIKA VIBAYA MNO.....
Ushauri wangu ni kwamba kuliko kuropoka na kuandika hovyo ni bora ukaripoti kwenye mamlaka husika.
 
Bahari ndo inajaa uchafu haswa
Sidhani kama samaki wanahusika na Cancer
Maoni yako mazuri mkuu,
Mimi na akili yangu ya kawaida ukichanganya na elimu yetu ya shule za serikali, tena zile za ufundi ambazo walifuta somo la baiolojia na jiografia nikasema baharini maji ni mengi mno inapunguza concetration ya sumu, pia yale machumvi ya baharini huenda kidogo yanapunguza nguvu ya sumu.

Muhimu hapo serikali ifanye tafiti na baharini.
Ahsante mkuu.
 
Ninahisi tu, hakuna haja ya kuwatisha watu.
Wakati naandika hili bandiko nilikuwa nakula hao samaki na nimetoka kupokea mzigo mwingine.

Pale ktk hoja kuu nimeshauri madawa ya mifugo, na mazao ya shamba yachunguzwe pia.

labda waende mbali na kuchunguza tabia za wahanga mfano matumizi ya vyombo vya plastiki kwa kuwekea vyakula vya moto, au kuweka juani inaweza kusababisha gesi za sumu zinazochangia saratani.

Matumizi ya madawa ya asili(mimea) ya mimea flani kupita kiasi huweza kusababisha saratani, wengi hili hatulijui lakini kuna mimea tunaitumia sana kama dawa za tumbo na vidonda kumbe ukizidisha ni hatari.
 
Elimu kuhusu madhara ya kemikali za migodini na dawa za kuua viatirifu Wananchi wengi hawana elimu ya kutosha. Wakazi wengi wa kanda ya Ziwa wanalima zao la Pamba na kitu ambacho ni kibaya wanachangamya na mazao mengine kama mahindi na maharage. Tatizo linakuja pale wanapotumia madawa makali kuulia viatirifu zinaathiri mazao kama Mahindi au Maharage pia kinaweza kuwa chanzo cha magonjwa mengi ya Kansa.
Pia kuna baadhi ya wakulima wanaolima mazao kama Kabeji(Cabbage) kando kando ya Ziwa wakati Kabeji zinachanua wanatumia madawa makali ya Pamba,wakati Kabeji inapojifunga dawa inakuwa ndani ya kabeji hadi inapokomaa.Hivyo basi kwa matumizi yasiyo sahihi ya madawa ya kuua viatirifu kwa mazao ambayo hayaitaji madawa makali au dawa ambazo zinachukua muda kupoteza makali nadhani pia inaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya Kansa.
Kuna ulazima wa hizi taasisi kutoa elimu na kufanya ukaguzi kila wakati ili kuondoa hatari za visabishi vya Kansa na pia Serikali/Bunge iwape fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya tafiti.
 
Bahari ni dampo kuu la taka chafuzi duniani hiyo ndio tofauti na hayo maji ya ziwa yana ishia baharini kupitia mto nile

Sasa ningependa tofauti hiyo ndio ukaihusisha na maudhui ya huu uzi.
Hilo ndio lengo hasa la kutaka utafiti ufanyike.
 
Mkuu umeleta hoja nzuri sana sana.
Matumizi ya madawa ya kuuwa wadudu shambani (sijui wanaita ni viwatilifu) na mbolea mbalimbali.

Kuna dawa flani ya copper imeuwa baadhi ya watu kwa saratani maeneo wanayolima kahawa. Wanatumia bila vifaa vya kujikinga kama gloves, mask, n.k.

Pia kuna mbolea flani sitaitaja sababu za kibiashara, imeandikwa wazi unapochanganya tumia mask na gloves maalum kuepuka madhara. Tatizo elimu ya wakulima wengi ni ndogo hupuuza haya maelekezo.
Ndani yake kuna phosphorus ambayo inasababisha matatizo kwa watoto ambao hawajazliwa kwa wamama wajawazito, au inaweza kuzuwia kuzaa kabisa, nadhani hii inaitwa teratogenic chemical.
Juu ya yote hii kemikali pia ni mutagenic, teratogenic or carcinogenic, nephrotoxic, myelotoxic, or pneumotoxic.

Kuna hoja pia ya watu kutumia madawa kama ngao ya kutibu vyandarua vya mbu kutibu magonjwa sugu ya zao la nyanya. Angalizo hii ni tuhuma inaweza kuwa ni uzushi tu.

Mtanisamehe kwa maelezo mengi na marefu mno lakini hii yote ni ktk kujadili na kuwahabarisha wenye dhamana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…