Serikali futa matokeo ya Form 4 badala yake tumia matokeo ya Mock, 2012

Sam Upendo

Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
32
Reaction score
10
Katika hali ya kawaida haiwezekani asilimia 60% ya watahiniwa wa form 4 wakafeli mtihani. Sote tunajua kwamba wanafunzi hawakufundishwa vizuri kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni mgomo wa kitaifa wa walimu mnamo mwezi wa saba japokuwa pilkapilka zake zilianza mapema kimya kimya bila kufundisha. Hivyo Serikali isipoingilia kati hali hiyo ili kunusuru maisha ya watoto malaika wasio na hatia itakuwa haikuwatendea haki.

Baada ya mgomo kufutwa walimu walienda Sensa, lakini hata waliporudi na shule zikafunguliwa walimu hawakufundisha kuwaandaa vizuri wanafunzi kwa ajili ya mitihani, hususan wale walimu ambao majina yao yaliondolewa kwenye orodha ya kuhesabu sensa dakika za mwisho kwa madai kwamba walikuwa vinara wa mgomo. Je, inawezekana kwamba walimu hao nao walichangia kwa kula njama za kulipiza kisasi katika usahihishaji ili kuikomoa Serikali? Inasikitisha kuona kwamba kuna wanafunzi waliokuwa wamepata Division 2 au 3 katika mock, lakini katika final wakafeli kabisa kwa Div 4 ya 35. Je, inaingia kichwani hiyo kwamba kufeli kwa wanafunzi kama hao ni halali yao?

Sasa ili kutenda haki na kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia nashauri serikali ikubali kufuta matokeo ya f4 yaliyotangazwa hivi karibuni, badala yake serikali itumie matokeo ya Mock, 2012. Hapo idadi ya kushindwa itakuwa ya kawaida, isiyotisha. Hatua hiyo ichukuliwe haraka iwezekanavyo ili watoto wachaguliwe kwenda f5.

Achana na mambo ya Tume ya kisiasa ambayo madhumuni yake ni kupoza hasira za wananchi, kwani sababu za kufeli zinafahamika.
 
jitihada zote hizo za nini na watu washafeli?
 
Kwani umeitwa kwenye tume?
Hujui mock shule zingine zinajitungia na kujisahihishia?
 
Nyie ndio mnataka kuturudisha nyuma kwa kufanya mambo kisiasa jitu linazero we unataka walipe 1, yambieni matoto na madogo yenu yasome yaache kuangalia tamthilia, waache kwendekeza ngono mtoto mdogo anawapenzi 8 afu unategemea lifaulu.

Ebu jaribu kumuliza huyo mtoto wako au jirani ako akwambie marais wangap wameitawala tanzania kwa sasa na mipangilio yao kwa miaka halijui, muulize mkoa wako unawilaya ngap na azitaje hajui afu unategemea afaulu,.

Hata we inaonyesha hujapita hata sekondari hamna four ya 35 au ulisoma wapi elimu yako,.

Tujiangalie watanzania kuhusu kuandaa hawa ndugu zetu sio kuilaumu serikali na walimu
 
Naomba kutoa mchango wangu; kwanza kabisa tusitenganishe matokeo haya wanafunzi (tusiseme wanafunzi hawahusiki) baada ya hapo ningependa ufahamu kwamba mitihani ya Mock haithaminiki kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, kuna baadhi ya wanafunzi hawajafanya hata Mock lakini Necta wamefanya, sasa unaposema yatumike matokeo ya Mock tutatoka nje ya lengo.. Kuna mtu alitoa report yenye majibu yaliyojibiwa na baadhi ya wanafunzi, tafuta ripoti hiyo utagundua kwamba tatizo ni kubwa sana! Toa wazo lingine ila hili la matokeo ya mock hapana
 
Visingizio vingi ni lazima tujue hii Certificate ya Form Four ni ya Kimataifa na sio ya Tanzania pekee na ndiyo maana vyuo vya nje vinatambua hivi cheti. Maswali ya Tanzania na yake ya shule Nigeria, UK, Canada ni sawa kwenye masomo ambayo yanatolewa kote. Pull ya maswali ambayo wanapewa wanafunzi yameshapitiwa na kupitishwa na watu ambao ni certified ya mashirika ya dunia ya System tunayotumia sasa ukweli ni kwamba elimu na kiwango kimeshuka. Hakuna umeme je wanafunzi watasoma vipi? hakuna walimu je wanafunzi watajifunza vipi, hakuna vitabu ye watoto watasoma nini?. kuwapa mtihani wa kiwango cha Form 2 haitasaidia kuongeza kiwango cha elimu. Ni wakati wa kusikiliza mawazo yetu badala ya kutafuta sababu.
 
Hayo maajabu ya kuwa na div4 ya point 35 yanaweza kutokea mwaka huu kwakuwa huu ni mwaka wa ajabu. Kama mtu hajafanya mtihani kafaulu paper sembuse huyo mwenye 35 kuwa na 4?
 
Wamefeli wengi na hawa sio wa kwanza
 
Tunapowatahini wanafunzi hatutafuti division I bali tunataka kujua ujuzi na maarifa waliyoyavuna wanfunzi hao kwa uwepo wao mashuleni. Kama wengi wameambulia SIFURI, basi inaonyesha wametoka kapa. Kwa hali hiyo taifa linapaswa kuwahoji wale waliojitwalia madaraka ya kusimamia maslahi ya taifa (including elimu) sababu za wanafunzi wengi kupata SIFURI.
 
Tupunguze mizaha kwenye suala la ELIMU kwa upande wetu ambao tulisoma kitambo tuwaone huruma hawa bongo flavour wetu maana media tulizonazo zinawaaminisha watoto hawa kuwa unaweza win maisha kwenye music, bongo movie, mpira n.k(hatujafikia huko ila kwa wenzetu wa Ulaya na Marekani ) Angalia vijana wetu jinsi wanavyo ongea, tenda utajua tu kuna tatizo la msingi katika jamii yetu tumewaaminisha katika maisha ya KUFIKIRIKA bila uwajibikaji na tumeruhusu siasa na wanasiasa kuchezea Elimu yetu. Walio athirika na ghalika hili ni watoto wa wadanganyika ambao tumewapeleka kwenye mapango ya kata tukiaminishwa na wanasihasa kuwa ni SHULE. Unategemea nini toka kwa mwanafunzi ambaye hajawahi ona maabara kufanya vizuri kwenye mtihani wa Chemistry, Biology, Physics????. Kwenye mapango hayo kumejaa waalimu wa vodafasta ambao matokeo yao hayakuwa mazuri lakini ndo waalimu wa watoto wetu???. Hata kama utawaambia warudie mitihani usitegemee miujiza kwenye matokeo hayo zaidi ya huruma ya kupewa alama za ufaulu ili serikali ipate sifa. Haya ni matunda ya kuaminisha wadanganyika kuwa elimu ni majengo na wanasiasa wa Tz walitumia karata hi iili wawe na cha kuonyesha kwa wapiga kura kwani wao wanaamini maendeleo ni katika vitu (tangible pekee), kupanga ni kuchagua tulichagua quantity dhidi ya quality so kizazi hiki kimekula kwao maana wazazi hamkusimama imara kutetea watoto wenu mlifurahia kanga, pilau, kofia na majengo so mnavuna mlicho panda. Tulijaribu kuwaambia hofu yetu kuhusu EAC lakini wakuu wa kaya wakasema siye ni waoga na wavivu pia si waaminifu sasa kwa hizi Div 0 na 4 tuna nafasi gani kwenye jumuia hii?????
Tupo kwenye Liberal society wazazi kuweni makini na malezi mnayowapa watoto wenu maendeleo tunayo yaona kwa wenzetu yanaendana na uwajibikaji sio kila tunachoona kwenye TV lazima nasi tukifanye vingine vinapingana na mila na desturi zetu
Si shangazwi na ukimya, je wadanganyika mnakumbuka kuwa mkulu alishaenda kufungua shule yenye mitaala ya Cambridge na kilometa chache kuna pango (shule ya kata) ambayo haina waalimu wa kutosha, maabara??????
TAFAKARI.
 

Mitoto ya siku hizi mingi imekalia Swaga tu haijutumi kusoma, nimesoma shule ya serkali na tulikuwa tunafundishana wenyewe kutokana na uhaba wa walimu.
 

kwa sheria ipi kutumia mock kwenda f5. we utakuwa gamba wanao wote na nduguzo wamefeli unasingizia walimi na kutoa ushauri wa kijinga kama huu.
 
Mtoto wako alipata div 1 kwenye mock??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kuna ambao hawakufanya mock wao tutatumia ya form 2 au?. haya mambo ya kuacha kufuata utaratibu kisa wanafunzi wengi wamefeli tuache .cha msingi ni tujielekeze kutatua matatizo yaliyopo ili hali hii isijirudie tena.walio kwama wanaweza ku resit au kuanza na certificate na still wakafanikisha malengo yao
 
We zuzu nini .watu washafeli unaongea madudu he! elimu sio tu unavyofikiria lazima ufikirie pia soko la kimataifa sio kuangalia tu mita chache.
 

napendekeza NECTA watunge pre-national ya kitaifa
 
MADESI;We zuzu nini .watu washafeli unaongea madudu he! elimu sio tu unavyofikiria lazima ufikirie pia soko la kimataifa sio kuangalia tu mita chache.

Mkuu angalia maneno yako vp?upo high level sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…