ni kweli kabisa tena walimu ambao hawajaajiriwa ni wengi wakiwemo waliotoka vyuoni directly ngazi zote na wale wa stashahada waliomaliza mwaka juzi na kufanya suplimentary mwaka jana wakafaulu lakini hawakuajiriwa. mfano wa uhakika nilionao ni chuo cha ualimu butimba watu 96 hawakuajiriwa, chuo cha ualimu bunda nilionana na watu tisa wakielekea dodoma kuomba ajira upya nao pia hawakuajiriwa, st john chuo kikuu cha dodoma ndo usiseme wapo kibao, kwa taarifa watu hao walitakiwa kwenda tamisemi kupeleka taarifa zao upya na wakaambiwa majina yao yatatoka kabla ya tarehe 1 ambayo ni leo na bado majina yao hayajatoka. kwa ujumla hili tatizo limekumba wengi na bado wanasubiri majibu yenye matumaini ya kuajiriwa tena.