Serikali haijali na kuwalinda wafanya biashara wa ndani

romaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
477
Reaction score
218
Ni aibu kabisa Kwa nchi maskini Kama Tanzania kumruhusu wafanya biashara wa nje Kama Wachina kuja kufanya umachinga Tanzania.

Sheria ya kulinda wafanya biashara wa ndani hapa iko wapi? Unakuta mfanya biashara wa ndani mdogo anaenda kununua Mzigo kiwandani china kuja kuuza Tanzania alafu wakati huo huo huyo mwenye kiwanda anakuja kuuza reja reja kwenye soko moja na huyo mchina.

Huu sio ushindani ni kuuwa na kuwazika wafanya biashara wa Tanzania wakiwa hai, serikali funguka nyie ndo mnatoa hizo leseni.
 

Mada yako nzuri sana lakini kwa wanzania inaweza kosa wachangiaji wa wazuri kwani watu wote wamejazana huko MMU na chit chat, subiri tuone
 
Haha kweli kabisa mkuu
 
dah! asante kwa kuliona hilo mkuu kiukweli selikali haipo ili kuwa support wazawa kwasababu hata mfanyabiasha mdogo tu anatozwa kodi kubwa kiasi cha kusababisha hata biashara kuteteleka na kiukweli tz kuna fursa nyingi za biashara but watu wanaogopa kujiingiza katika mfumo wa biashara kutokana na sheria kandamizi za serikali tz!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…