Serikali haikusanyi kodi

Serikali haikusanyi kodi

Kagosaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2010
Posts
208
Reaction score
56
Ninasikitishwa sana kuona kwamba huku tunakoelekea siko kabisa.

Nyumba za Masaki, Oysterbay, Ada Estate na pale Kinondoni waliuziwa vigogo wa serikali. Tulikuwa na matumaini kwamba wange kaa huko. Ajabu ni kwamba nyumba hizi kwa sasa zimepangishwa / zinapangishwa kati ya USD. 3,500 na USD. 15,000 na zaidi kwa mwezi.

Kwa sasa ofisi binafsi na zile za kimataifa zimepanga katika nyumba hizi. Wakubwa hawa hawalipi kodi. Wamiliki wengi wa nyumba za Dar es Salaam pia hawalipi kodi. Mfano, kule Ilala kuna mtu ana nyumba 40, zinapangishwa kati ya laki 2 na laki nne! Kiwanja hakijapimwa, na serikali inapoteza kodi kibao!

Ndo maana kila wakati serikali inaomba pesa za maendeleo badala ya kutumia vyanzo tulivyonavyo! Tunataka serikali ikusanye kodi..
 
umeongea vizuri mzee!
lakini hapo inaonekana kam umemkamia huyo jamaa wa ilala peke yake....amekupiga kodi ya juu nini!!!
kama viwanja havijapimwa, na serikali haina mpango huo, mtu atalipaje kodi, au akajipimie kiwanja mwenyewe?
k
hata hivyo kuna maeneo meeeengi tu ambayo yanahitaji kusimamiwa vizuri. shida kubwa ni kwamba hata wakizikusanya huzipeleka kuzificha nje, wao wanaita vijisent
 
Huyo wa Ilala ni mfano tu, kama zilivyo nyumba za kule Masaki, Oysterbay na Ada Estate, ila serikali lazima ikazane kukusanya kodi. Kutokusanya kodi ni dalili za rushwa!
 
What about wale walionunua mijengo ya serikali sasa hivi wametafuta wabia wanaporomosha magorofa kama pale ADA ESTATE opposite St Peters imekaaje hii? :A S angry:
 
Mwalimu alikwishasema, serikali corrupt haitozi kodi. ukiona hivyo, ujuwe serikali, yaani sisi watz ni corrupt, ndo maana hatuna uwezo wa kutoza kodi. kazi ni kwetu sasa.
 
What about wale walionunua mijengo ya serikali sasa hivi wametafuta wabia wanaporomosha magorofa kama pale ADA ESTATE opposite St Peters imekaaje hii? :A S angry:

Halafu, hakuna hata ufuatiliaji kwamba kama jengo limekuwa storey building basi kodi ipandishwe... Pia hayo walioyapangishwa nayo hayatozwi kodi. Kila siku tunalalamika tu kwamba serikali haina hela, mimi nasema hela ipo ila hakuna strategy ya kukusanya kodi.
 
Mwalimu alikwishasema, serikali corrupt haitozi kodi. ukiona hivyo, ujuwe serikali, yaani sisi watz ni corrupt, ndo maana hatuna uwezo wa kutoza kodi. kazi ni kwetu sasa.[/QUOTE}

Sio kwamba wote ni corrupt, ila hatusikilizwi na yawezekana serikali haisikilizi pia mchango wa watalaam (think tanks).
 
Mi naona vyanzo vya kukusanya mapato nchi hii ni zaidi ya pango la nyumba, usipige tu mayowe ndugu yangu maana siku wakiweka sheria kuwa nyumba lazima ikipangishwa ilipiwe kodi nakuambia maskini hataweza kusihi mji huu wa Dar maana kodi itakuwa haikamatiki.Cha msingi serikali iangalie vyanzo vingine vya mapato na kama ikiamua kuwatoza kodi wapangishaji wa nyumba basi ihakikishe imetengeneza makazi kwa watu maskini then anaepanga sasa imtoze kodi maana atakuwa ni tajiri
 
Hahaa!
Mwenye nyumba huyo,
MAana povu lilivyo mtoka inaelekea tena ni zile za serekali kapamngisha!
 
Back
Top Bottom