Serikali haina uhalali wa kumfukuza Mtumishi wa Umma kwa kuwa na madeni kama yenyewe kila siku inadaiwa mpaka mali zake kukamatwa

Serikali haina uhalali wa kumfukuza Mtumishi wa Umma kwa kuwa na madeni kama yenyewe kila siku inadaiwa mpaka mali zake kukamatwa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa mujibu wa sheria/taratibu za Utumishi wa umma, mfanyakazi kuwa na madeni kupitia kiasi ni jambo linaloweza kuhatarisha ajira yako serikalini.

Binafsi najiuliza, serikali ambayo yenyewe ina madeni mengi yakiwemo ya watumishi wa umma mbali na ya makampuni binafsi, inapata wapi uhalali wa kutekeleza sheria ya kumuwajibisha mtumishi wa umma kwa madeni?

Kama mtumishi mwenye madeni anaitia doa serikali au taasisi anayofanyia kazi, serikali kudaiwa mpaka mali zake kukamatwa huko nje ya nchi si kulitia aibu Taifa zima?

Itakuwa sahihi kama viongozi wanaofanya maamuzi yanayoiingiza nchi katika madeni ya aibu na wao wawajibishwe kama ilivyo kwa watumishi wa umma.

Sheria inapaswa kuwa ni msumeno na sio kisu cha kawaida.
 
Back
Top Bottom