Serikali hakikini taaluma za wachungaji na masheikh ili kulinda heshima ya watanzania juu ya waovu na matapeli

Serikali hakikini taaluma za wachungaji na masheikh ili kulinda heshima ya watanzania juu ya waovu na matapeli

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Wazo kuu.

Hili wazo mlifanyie kazi, Kwa maslahi mapana ya nchi zetu, ni kweli katiba ya nchi inatambua uhuru wa kuabudu,
Lakini serikali kupitia taasisi zake mnafaa kuangazia hilo kwani itasaidia kulinda utu wa mtanzania kutikana na viongozi wa dini wenye tamaa ambao huishia kuwatapeli wananchi na wengine kubaka na kulawiti waumini wasio na hatia.

Kwa kuanza kwanza wamiliki wa ministries, makanisa walau wawe na shahada ya theolojia, na wale wanaotumia majina ya ministries nyingine wawe na walau Cheti cha theolojia kutoka vyuo vinavyotambulika iwe ndani ya nchi au nje ya nchi, hii itasaidia kuwabaini wajanjawajanja wachache walioingia kwenye dini kuumiza wengine.

Chunguzeni pia taasis za kidini Kwa umakini na wanafanya nini kwani bila kufanya hayo taifa litazidi kupotea kimaadili huku mkiwa mnawaangalia.

Hapa hakuna kulaumu maana viongozi wote wawe wakristo, waislamu imetokea wimbi kubwa la utapeli, ubakaji na ulawiti na mmekua mkifumbia macho hayo mambo sio sawa.

Kwa kuongezea mnaweza kwenda kujifunza nchini Rwanda wao walifanya nini ili kurudisha nchi yao kwenye mstali sahihi.
 
Kwa upande mwingine Mungu akimtumia mtu hahitaji kitu kinachoitwa Theology,
Hilo la kwanza elewa kuna watu hawakusoma theology na wakawa moto tena wengine hata shule hawakwenda kabisa akiwemo Mtume Petro hapo kale na miaka ya juzi ni William Branham na wengine wengi
Maswala ya Imani ni Maswala ya ajabu sana na complicated!
 
Hujasema maimaamu wawe na elimu gani na Masheikh wawe na elimu gani?
Dini zote waislamu na wakristo wahakikiwe sio maimamu, maustaadhi, masheikh, wachungaji, makatekista, mapadre, maaskaofu hiyo itaweka usawa na government intervention will save a great society ambayo hali huko ni mbaya sana na watu wanaumizwa mno
 
Back
Top Bottom