Serikali hamisheni dampo la Pugu Kinyamwezi

Serikali hamisheni dampo la Pugu Kinyamwezi

Joannah

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2020
Posts
20,921
Reaction score
49,014
Viongozi wenye dhamana katika hili,nawasalimu!

Jana jioni mida ya saa moja nilipita mitaa ya PUGU KINYAMWEZI, nilistushwa na moshi uliotanda kwenye mazingira Yale nyumba zote zimezingirwa na moshi mithili ya ukungu wa usubuhi kwenye safu za milima ya Uluguru.

Kiukweli, mimi tu mpita njia Tena ndani ya gari nilisikia harufu ya moshi ule haikuwa mzuri,unanuka!Hali Ni mbaya sana.Nikijaribu kuvaa viatu vya wananchi wale havikunitosha. Hivi tumeshawahi kufikiria madhara ya huo moshi kwenye mwili wa binadamu? Kuna watoto, wagonjwa, wazee wote wanavuta hewa Ile kweli? Kwa mawazo yangu tu nahisi Kuna kila aina ya taka hasa plastic kwenye moshi huo japo sijaziona taka kwa macho yangu.

Lengo la Uzi huo kuiomba Serikali kuhamisha hilo DAMPO jamani mbona Dar es Salaam Kuna mapori mengi tu bado, litafutwe eneo hilo dampo lihamishiwe huko

Hii tabia ya kupuuzia Mambo muhimu kàma haya tutaja tengeneza kizazi chenye maradhi yasiyotibika...Ni matumaini yangu serikali yetu sikivu italifanyia kazi..,Mheshimiwa Amosi Makalla pambania hili,na Baba Phillip Mpango pambania jirani zako.
 
Siyo kwamba watu ndiyo wamelifuata hilo dampo, hapo shida ni mamlaka za upangaji miji kutotekeleza wajibu wao wangekuwa wanatekeleza sidhani kama makazi ya watu yangekuwa around eneo la dampo same case ya huko ni sawa na machinjio ya vingunguti ile harufu ni mbaya isiyo vumilika ila watu wanaoishi kule wala huoni wakipata shida na harufu huenda sense za harufu zimeshaathirika.
 
Hata wakihamisha Bado shida itakuwa ileile, mwanzoni ilikuwa Tabata wakati huo Tabata ni pori watu wakahamia malayalam yakaanza ikabidi lihamishwe pugu watu wakalifata.
 
Wakati dampo lina hamishiwa huko. Kulikuwa ni mapori, watu wameongezeka wamejenga mji umekua hadi wamelifikia dambo na kulizingira.

Hata wakilihamishia visiga watu watafika tu..chamsingi serikali, ijenge sanitary landfills ambazo zipo standard ili kuepuka madhara ya kiafya na kimazingira.

Dampo la pugu kinyamwezi ni moja kati ya aibu kubwa kwa jiji la dsm.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hata wakihamisha Bado shida itakuwa ileile, mwanzoni ilikuwa tabata wakati huo tabata ni pori watu wakahamia malayalam yakaanza ikabidi lihamishwe pugu watu wakalifata
Sawa litahamishwa pia.Miji inakuwa hatuwezi kuzuia hilo
 
Wakati dampo lina hamishiwa huko..kulikuwa ni mapori..watu wameongezeka wamejenga mji umekua hadi wamelifikia dambo na kulizingira.

Hata wakilihamishia visiga watu watafika tu..chamsingi serikali..ijenge sanitary landfills ambazo zipo standard ili kuepuka madhara ya kiafya na kimazingira.

Dampo la pugu kinyamwezi ni moja kati ya aibu kubwa kwa jiji la dsm.

#MaendeleoHayanaChama
Yess!haya ndio maneno Sasa,wajenge hicho kitu ulichosuggest.....yaani ungeona nilichokiona Jana ungestaajabu kabisa
 
Usiombe mvua inyeshe huo Moshi sijui ni mvuke sijui ni harufu inafika hadi Jk Nyerere airport , wanuka sana yani wanaokaa karibu na hilo dampo baada ya miaka kadhaa hospital zitakosa sehemu za kulaza watu kwa maradhi sugu.
 
Back
Top Bottom