#COVID19 Serikali: Hatujabaini Kirusi cha Omicron mpaka sasa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Serikali imesema Maabara ya Taifa imekuwa ikichunguza mabadiliko ya kirusi ili kuangalia uwepo wa anuai zinazotokana na mabadiliko ya COVID-19, ikiwemo Omicron na mpaka sasa haijabaini aina hiyo mpya ya Kirusi

Imesema haijajulikana kama abiria kutoka Tanzania aliyeripotiwa kubainika na Kirusi cha Omicron huko Delhi Nchini India Desemba 05, 2021 alitokea Tanzania moja kwa moja au alipita kuelekea India

Wananchi wameendelea kusisitizwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na Maji tiririka, kuvaa Barakoa, kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima na kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya

D0F093D7-E896-4CBA-88EE-581FC37FAC09.jpeg

F4A56622-4B9F-4C91-B465-F01F3FC8F7EC.jpeg
 
hata cha Rona pia hakuna ni kutishana na kubambikiziana tu kama yalivyo mazoea yetu..kubambikiziana...! Ugaid,i uhujumu uchumi na menginetele tu.
 
Mchaka mchaka, Hakuna Corona.....CHINJA😆
 
Hii itakua na chanjo yake mpya ama itakuaje?

Mwakani December itaibuka variant nyingine.

Hadi 2025 ndio corona itaisha, litaibuka gonjwa jipya.

Corona is a hoax.
 
"Wanasema tusimamishe shughuli. Mishahara yao itatoka wapi sasa?" -- alisikia mwendazake akikomelea.

Ngoja wapiga pesa wafanze yao kwanza mengine tutajuana mbele kwa mbele:

Tanzania na Hadaa kwa Dunia
 
Serikali imesema Maabara ya Taifa imekuwa ikichunguza mabadiliko ya kirusi ili kuangalia uwepo wa anuai zinazotokana na mabadiliko ya COVID-19, ikiwemo Omicron na mpaka sasa haijabaini aina hiyo mpya ya Kirusi

Imesema haijajulikana kama abiria kutoka Tanzania aliyeripotiwa kubainika na Kirusi cha Omicron huko Delhi Nchini India Desemba 05, 2021 alitokea Tanzania moja kwa moja au alipita kuelekea India

Wananchi wameendelea kusisitizwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na Maji tiririka, kuvaa Barakoa, kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima na kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya

View attachment 2034493
View attachment 2034494
Wa msamon balozi wa India na US kwa kutuchafua
 
Ngoja likiwekwa fungu la mgao wa pesa kupambana na Omnicron tutakipatam..sasa hivi hakina manufaa😁
 
Waendelee kuwa viherehere kuchunguzi kirusi yatawakuta ya South Africa, kufungiwa milango
 
Back
Top Bottom