The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo amesema wizara walitoa mwongozo wa mabasi ya shule na kwamba waliviachia vyombo vingine vya Serikali kuendelea na ukaguzi wa madereva hao kama wanavyofanya kwa madereva wengine na hawakuwahi kuwa na mfumo.
“Baada ya uzoefu huu tutatafakari, namna gani nzuri tutaangalia dereva yupi atafaa kubeba watoto ni suala ambalo sasa tulifikirie kwa umbali zaidi kama Serikali tunapaswa kufanya nini katika suala hili.
“Katika mifumo ya kiserikai tayari dereva awe amekidhi vigezo lakini sasa utahitajika ukaguzi zaidi kwa madereva wa watoto, kulitafakari kwa pamoja na vyombo vingine na kulitolea msimamo. Kama kutakua na uhitaji wa kuongeza sifa za ziada kupitia mifumo ya serikali,” amesema Profesa Nombo.
Miongoni mwa ajali hizo ambazo inadaiwa imesababishwa na uzembe wa dereva ni ya gari Toyota Hiace la Shule ya Msingi Ghati Memorial, kuangukia kwenye korongo lililojaa maji eneo la Dampo mkoani Arusha.
Katika maelezo yake, Profesa Nombo amesisitiza ili dereva aweze kukabidhiwa gari la wanafunzi lazima awe na vigezo na kazi ya trafiki ni kuwakagua kama wana vigezo na kupitia mchakato wa kuwa dereva.
“Madereva wanaobeba watoto wa shule, wanapaswa wawe makini zaidi tunategemea aliyekabidhiwa jukumu hilo, atazingatia kulinda uhai wa wale anaowabeba,” amesema.
Mwongozo
Waraka wa Elimu Na. 01 wa mwaka 2023 kuhusu uboreshaji wa huduma ya magari au mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi, ulioanza kutumika Machi Mosi 2023 ulielekeza umakini kwa wamiliki wa shule kwa kuwa kuwa thamani ya rasilimali watoto ni kubwa kuliko thamani ya rasilimali yoyote ambayo nchi imejaliwa kuwa nayo.
Waraka huo uliolenga kuboresha utoaji wa huduma ya usafiri wa magari na mabasi kwa wanafrunzi uliwataka kuzingatia kutokuwepo kwa viashiria vyovyote vya ukatili dhidi ya wanafunzi ikiwemo ubakaji na ulawiti na tabia zenye viashiria vya mmomonyoko wa maadili.
“Tabia hizi zinaleta mmomonyoko wa maadili, kuathiri ukuaji, ujifunzaji na kuhatarisha ustawi wa watoto kwa ujumla. Haitakiwi kuwa na wahudumu jinsi moja ya wanaume pekee, kuweka miziki au nyimbo au picha za video zisizozingatia maadili, mila na destrui na tamaduni, kuwafanyia vitendo vya ukatili,” ulielekeza.
Mwongozo huo uliosainiwa na Kamishna wa Elimu, Dk Lyabwene Mtahabwa ulielekeza shule kuwa na ratiba rafiki za safari ili wanafunzi hususani watoto wadogo wapate muda wa kutosha kupumzika kwa ajili ya ukuaji wao.
Pia, uliekeza kuwa na mabasi yenye vioo angavu, wamiliki kuhakikisha wanaowaajiri wawe waaminifu, wenye weledi na maadili.
“Endapo mhudumu yeyote ataenda kinyuma na maadili au kuhatarisha usalama wa wanafunzi, mmiliki wa shule achukue hatua mara moja dhidi ya mtumishi husika.”
PIA, SOMA:

- Wanafunzi Saba wahofiwa kupoteza Maisha baada ya School Bus kuanguka kwenye korongo (Sinoni, Arusha)
- Rais Samia: Serikali kufanya uchunguzi sababu halisi za mafuriko na kuchukua hatua
- Arusha: Rais Samia ashiriki Misa Maalum ya Miaka 40 ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine. Atoa pole kwa familia za wanafunzi waliofariki
- Katavi: Mabasi ya Wanafunzi yabainika kufungwa mipira kwenye mfumo wa breki
- Arusha: Jeshi la Polisi laendelea na ukaguzi wa mabasi ya Shule ili kubaini magari mabovu na kuyazuia
- Mbeya: Wamiliki wa Shule watakiwa kuhakikisha 'School Buses' zikakaguliwa na Polisi kabla ya kubeba Wanafunzi