Serikali iache kusambaza umeme vijijini, wajikite katika uzalishaji umeme

Serikali iache kusambaza umeme vijijini, wajikite katika uzalishaji umeme

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Sasa ni wakati wa kuachana na kusambaza umeme vijijini Ili fedha hizo zitumike kujenga vyanzo vya umeme kwani huwezi sambaza kitu ambacho huna.

Hii italeta tija, sio kepeleka feza za kuwasha taa na mgao huu
 
We dogo una umri gani kwani! Kwa akili hii unapaswa kuwa chini ya miaka 18...humo kichwani ni 00 kabisa
 
huoni usambazaji umeme vijijini umerahisisha shuhuri za kiuchumi vijijini na kupunguza utegemezi wa shuhuri za kiuchumi mijini watu wakivuna mazao ni rahisi kwa sasa kuondoa makapi kwa kupitia viwanda vidogo vijijini kwa mfano kusaga mahindi na kukoboa mpunga,kusindika matunda na ata kukuza vijiji na kupunguza makali ya ajira vijijini na kingine kurahisisha upatikanaji wa habari na ata huduma za afya vijijini na shuhuri nzima za utendaji vijijini.
 
Inaonekana mtoa mada unaishi mjini,halafu mjini kwenyewe umeenda ukiwa mkubwa tayari ukitokea kijijini...
 
Kumbe Jf kuna watu wajinga sana,nashangaa kuona watu wote waliochangia uzi ni wajinga kiasi hiki wana mu attack mtoa mada pasipo hata kufikiria.
Mtoa mada assumption yako IPO very true,huwezi kusambaza kitu ambacho huna ni bora Serikali iwekeze kwanza nguvu kwenye uzalishaji.Imagine huu ukame ukazidi hata miaka 2/3 mfululizo huo umeme utaupata wapi?
 
Back
Top Bottom