Serikali iache kuwadhalilisha walimu kwa kugawa vishkwambi, waboreshe maslahi yao ili wanunue wenyewe!

Serikali iache kuwadhalilisha walimu kwa kugawa vishkwambi, waboreshe maslahi yao ili wanunue wenyewe!

A HUMBLE LEADER

Senior Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
138
Reaction score
343
Serikali ya CCM

Acheni kutudhalilisha makada waaminifu kama sisi KWA hoja za hovyo zisizo na afya KWA Taifa!

Hivi mnafikiri vishkwambi KWA walimu;-

1.Vitaongeza maslahi yao ya kazi!?

2.vitawapa unafuu wa mfumuko wa bei ya chakula na mahitaji mengine!?

3.vitawapandisha madaraja wale waliofundisha KWA muda MREFU bila kupanda au kupanda mara MOJA tu ndani ya miaka 9 kama waajiriwa wa mwaka 2014!!?

4.vitaongeza mzunguko wa fedha KWA walimu na kufurahia Maisha yao!!?

Acheni majibu mepesi KWA maswali magumu!

Acheni kukidhalilisha chama kwamba kimekosa think tank Hadi kuja na hoja mfu kama hizi!!!

Kama mmeshindwa cha kufanya uzeni vishkwambi muwape fedha wakale kuliko kufanya siasa mfu kama hizi!

Walimu siyo Watoto msiwatie hasira kali wakahujumu ufundishaji wao!

Rudini chimwaga mjipange tena hicho mlichokuja nacho sio TIJA KWA walimu bali udhalilishaji wa watumishi wa umma!!
 
Shukuru kwa chochote hata kama ni kidogo sana, itakua ni mwanzo mzuri wa kushukuru hata kikubwa siku kikiwajilieni.
 
Shukuru kwa chochote hata kama ni kidogo sana, itakua ni mwanzo mzuri wa kushukuru hata kikubwa siku kikiwajilieni.
Washukuru KWA dhihaka za Chama!? Au washukuru KWA kipi hasa Zaid ya kudhalilishwa!!?
 
Washukuru KWA dhihaka za Chama!? Au washukuru KWA kipi hasa Zaid ya kudhalilishwa!!?
sijaona walipodhalilishwa, na kimsingi katika kuendea malengo ya millemiun goal no. 4 ni Digitizing and empoworing quality education. Na kua na gadgets kama laptops na tablets ni njia ya kuelekea huko mkuu.

Ndio serikali inamapungufu yake mengi tu ila sijajua kwanini umeitafsiri hatua hii ya kugawa tablets kwa walimu kama "udhalilishaji" Hebu fikiri upya juu ya nadharia yako.
 
Wale walio pewa mwazo means makalani mbona hamkusema wamedharirishwa?
 
sijaona walipodhalilishwa, na kimsingi katika kuendea malengo ya millemiun goal no. 4 ni Digitizing and empoworing quality education. Na kua na gadgets kama laptops na tablets ni njia ya kuelekea huko mkuu.

Ndio serikali inamapungufu yake mengi tu ila sijajua kwanini umeitafsiri hatua hii ya kugawa tablets kwa walimu kama "udhalilishaji" Hebu fikiri upya juu ya nadharia yako.
Mjinga tuu huyu. Sijui him roho mbaya kaitoa walk?
 
Shukuru kwa chochote hata kama ni kidogo sana, itakua ni mwanzo mzuri wa kushukuru hata kikubwa siku kikiwajilieni.
Mkuu hivyo vishikwambi sio kuwa wamepewa viwe vyao bali ni mali ya serikali na vina nembo ya taifa na sharti ni kuwa ukihama au ukistaafu lazima ukirudishe.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom