Serikali iajiri walimu wa sekondari na msingi, hali ni tete mashuleni

Serikali iajiri walimu wa sekondari na msingi, hali ni tete mashuleni

Teleza1

Senior Member
Joined
May 16, 2020
Posts
190
Reaction score
198
Kwa heshima na taadhima naomba kuhufahamisha umma changamoto mbalimbali tunazopitia mashuleni nahisi kama serikali haijui au na kama inajua na imeamua kukaa kimya hali mashuleni mbaya sasa hivi vipindi vinamalizika mashuleni saa 11 mpaka 12.

Kwa hiyo mwalimu au waalimu tuna toil kinyama bora hata waalimu wa arts angalau wenyewe wako wengi ukilinganisha na idadi ya waalimu wa sayansi, mimi nafundisha Mathematics na Physics kuanzia form one mpaka four niko wima kuanzia asubuhi mpaka jioni

Plz naomba serikali iongeze waalimu wa sayansi ili itupunguzie adha sisi waalimu wa sayansi.

Mhe. Rais alisema kuna ajira zaidi ya 10000 kwa waalimu nilifarijika na kajipa moyo kwamba kwa ongezeko hilo teaching load inaweza kupungua lakini mpaka sasa hivi kimya plz mheshimiwa rais naomba utupunguzie adha, mimi ni mzalendo na naipenda kazi yangu.
 
Wastani wa vipindi ni 28 au 24 nadhani kwa wiki,wewe fundishwa hivyo ,vitakavyozidi muachie mkuu na mtaaluma wake,tatizo Nini sasa,acha kulalamika.
 
Wameshindwa kuajiri polisi wasaidie kusimamia uchaguzi ndio waje kuajiri walimu ambao juzi tu mlikuwa likizo ya corona. Piga kazi
 
Ndio hii serikali inayosifiwa kila siku? Tena kuwa makini wasisikie ukilalamika unaweza ukavunjwa miguu.
 
Kama hatua za haraka hazita chukuliwa katika miaka michache ijayo Tanzania haitakua na wataalamu yani engineers physics haina tena walimu vijana wanafeli na wanaikimbia !!! Acha tuajiri wanajeshi ttuuu kukoka jkt jibu tutalipata
 
Elimu saivi sio kipaombele kwa CCM kwa hiyo tulia, kuajili sio kipaombele saivi, tunajili wa jeshi tuu

Ila poleni sana walimu wetu maana kazi mnaipata kila upande, sio kiuchumi wala kwa kazi

Chapa kazi tunaenda vizur usitishwe na mabeberu
 
Unaijua physics na maths au unaropoka tuuu!??
Hoja sio kuijua,fundishwa kwa mujibu wa vipindi vyako kwa wiki,Kama 24 au 28,vingine una haki ya kukataa,wizara imeweka ukomo wa vipindi kwa wiki, maximum ni 28,sasa Kama unalazimishwa kumfundisha zaidi ya hapo,ujue hufahamu haki yako.
Kuwa na msimamo mwalimu,Kama uko private sawa,Ila Kama uko serikalini, fanya hivyo.
Usione wewe ndo mwalimu pekee,Kuna walimu wengine wako humu Ila hawajitangazi,wanakuelekeza,unajua mjuaji, acha hizo utaumia.
Hakunaga sifa kwenye kazi za utumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom