Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 208
- 91
Kumekuwepo na usumbufu mkubwa sana kwa abiria wanautumia huduma za mabasi ya mwendokasi. Abiria anapokata tiketi anaambiwa hakuna chenji asubiri mpaka itakapopatikana, hii ni sawa kweli? Huduma ya namna hii? Kama hawana uwezo wa kuwa na hizo chenji za Tshs 50 waondoe hiyo Tshs 50.
Najiuliza hizi chenji zinazoachwa na mamia ya abiria zinaenda wapi? zinakua za nani? nani anafaidika nazo? au ndio wahudumu wanaokatisha tiketi wanajikusanyia mitaji?
Hii sio sawa na haikubaliki kabisa, maana wao ikitokea abiria amepeleza hiyo Tshs 50 hawawezi kumpatia tiketi wala kumruhusu aingie kituoni, sasa iweje Tshs 50 za abiria wazione hazina kazi wanakua wanajikusanyia tu wanabaki nazo?
Mamlaka zinazohusika zichukue hatua tafadhari kwa sababu sio suala la dharura ni kitu kinaeleweka kabisa kuwa chenji zinahitajika.