Serikali iangalie hili la Zahanati ya Kongowe Kibaha kuwadai wajawazito Sh 20,000 kwa lazima

Serikali iangalie hili la Zahanati ya Kongowe Kibaha kuwadai wajawazito Sh 20,000 kwa lazima

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Kuna Zahanati ya Serikali ipo Kibaha Kongowe inaitwa Zahanati ya Kongowe ipo karibu na Shule ya Msingi Kongowe, mama mjamzito akienda kuanza kliniki anaombwa Shilingi 20,000 kwa lazima, kiasi ambacho hakipo kwenye mahesabu yoyote ya huduma.

Ikitokea aliyeombwa hana au amekataa kutoa wanamkufukuza, tunaomba mtusaidie kututangazia kero hiyo.

DIWANI AKANUSHA TUHUMA
Alipoulizwa kuhusu tetesi hizo, Diwani wa Kongowe, Hamis Shomari amesema “Hizo taarifa si za kweli, mimi mwenyewe mke wangu anafanya kazi katika hiyo zahanati, sijawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo.”
 
Back
Top Bottom