Nafikiri ipo haja pia kwa jamii kurudisha ule utaratibu wa zamani wa kusaidiana watoto;
Kama dada yako au kaka yako anachangamoto ya kiafya au hata ya kiuchumi; msaidie mtoto hata mmoja kumlea.....Kwa wanao amini vitabu vya Mungu unakuwa umefanya jambo jema sana, sana sana.
Unakuta mtu kila kukicha anamwaga vyakula, wakati watoto wa dada yake wana lala njaa; Mchukue mtoto hata asome shule ya kayumba ni poa tu kwani atapata uangalizi na atakula vizuri