DOKEZO Serikali iangalie suala la vigezo vya wanaosomea Ufamasia, taaluma hiyo inakoelekea siko

DOKEZO Serikali iangalie suala la vigezo vya wanaosomea Ufamasia, taaluma hiyo inakoelekea siko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kadodo1

Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
25
Reaction score
24
Moja ya changamoto ambayo imekuwa ikitawala kwenye midomo ya Watanzania wengi ni kuhusu suala la Wahudumu wa maduka ya dawa hasa yake ya mtaani.

Kumekuwa na changamoto ambazo Wananchi wanaoenda kununua dawa wanadai wanakutana na watu ambao uelewa wao kidogo ni changamoto.

Mimi mwenyewe imewahi kunikuta, unamuelekeza kitu fulani lakini kwa jinsi anavyokujibu ni wazi unabaini huyu muuzaji hana uelewa wa kiwango hicho wa kile anachokifanya.

Uuzaji wa Dawa sio kazi ya kumwambia mtu yeyote kwamba simama hapo niuzie, bei ya dawa hii ni kiasi fulani n.k Inahitajika taaluma na mhusika awe na uelewa kwa kuwa hapo unazungumzia afya, maisha ya mtu au watu.

Kwa kuwa nina uzoefu kidogo kwenye sekta hiyo nina hoja kuhusu vigezo au elimu ya wanaofanya kazi hiyo.

Hivi karibuni nilisikia kuwa Serikali inataka kuongeza vigezo kwa maana ya kuboresha vigezo vya wahusika wanaohitaji kusomea Ufamasia wawe navyo katika vyuo vya kati.

Vigezo zinavyotarajiwa ni vinavyowataka wanafunzi kuwa na ufaulu elimu ya Sekondari kwa alama D tano za masomo ya Fizikia, Baolojia, Kemia, Kingereza na Hisabati kutoka alama D mbili za Baolojia na Kemia zinazotumika sasa.

Nilipata nafasi ya kuyajua hayo niliposhiriki moja ya session za mafunzo ya afya ngazi ya kati.

Nadhani kuna haja ya kufanya mabadiliko hayo ili angalau Jamii ipate watu ambao kichwani watakuwa wamechangamka kwa kiasi fulani, inawezekana kanuni za kutumia D mbili zinaweza kuwa zinachangia kupatikana kwa watu mbao wanashindwa kujiongeza kielimu.

Taaluma ya famasia ni moja ya taaluma muhimu, kuendelea kuichekea ni kuzalisha magonjwa sugu, vifo na ikiwezekana kutengeneza kizazi mbacho hakijui matumizi ya dawa.

Jambo hili linaweza kuwa gumu kwa baadhi ya watu kulielewa hasa wale wenye maslahi binafsi, wale wanaomiliki vyoo vya Ufamasia na wamiliki wa maduka ya dawa, watajua kuwa huu unaweza kuwa mwanzo wa kuwaharibia biashara zao.

Wanaweza kupinga hata hii mada lakini hii sifanyi kwa faida yangu wala familia yangu bali Wanzania na watu wote kwa jumla wanaohudumiwa na Wafamasia.

Mtaalamu wa afya akikosea maisha ya mtu hayawezi kurudishwa kwa vyovyote vile.

Vigezo vipya pia vitawapa fursa wahitimu wa stashahada ya famasi kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi kuliko ilivyo sasa, ambapo wao wakimaliza wanaona maksi walizopata zinawatosha.

Pia itawawezesha kukubalika kwenye soko la kimataifa, na kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wenye umahiri wa kufanya kazi kwenye viwanda vya dawa.
 
Back
Top Bottom