Serikali iangalie upya maternity leave badala ya miezi 3 iwe miezi 5 au 6

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955
Malezi ya mtoto mchanga yanahitaji uangalizi mkubwa sana wa mama yake! Nashangaa serikali mnasisitiza mtoto asipewe maji wala uji ndani ya miez 6! yaani awe anashindia maziwa ya mama tu!

Nyinyi hao hao serikali mnawapa wafanyakaz wenu miez 3 tu ya materninty hamuoni tatizo kwa watoto kuwa badae wanakuwa na mapungufu mengi kwa kukosa malezi?

Miezi 3 maana yake mtoto aanze kupewa uji ili kukidhi mahitaji maana mama yake anakuwa kazini! mnalazmisha watoto kukomaza utumbo mapema.

Ni wakati sasa sera zibadilike kunyonyesha ni miez sita na leave iwe miez 6, tulinde vizazi vyetu ili baadae wawe watoto bora wala sio bora watoto!
 
Kuna vifaa vya kuhifadhia maziwa ya mama pindi anapokuwa mbali na mtoto na mtoto akatumia kwa muda ambao hayupo na mama. Unayahifadhi kwenye jokofu kwa ajili ya mtoto awapo mbali na mama.

Nashkuru mwanangu yupo na mama yake 24/7.
 
Vifaa magonjwa bakteria kibao! mama anapotea masaa 6 anapita kuvuja tu maziwa kazini huko!
Kuna vifaa vya kuhifadhia maziwa ya mama pindi anapokuwa mbali na mtoto na mtoto akatumia kwa muda ambao hayupo na mama. Unayahifadhi kwenye jokofu kwa ajili ya mtoto awapo mbali na mama.

Nashkuru mwanangu yupo na mama yake
 
Malezi ya mtoto mchanga yanahitaji uangalizi mkubwa sana wa mama yake! Nashangaa serikali mnasisitiza mtoto asipewe maji wala uji ndani ya miez 6! yaani awe anashindia maziwa ya mama tu!

Nyinyi hao hao serikali mnawapa wafanyakaz wenu miez 3 tu ya materninty hamuoni tatizo kwa watoto kuwa badae wanakuwa na mapungufu mengi kwa kukosa malezi?

Miezi 3 maana yake mtoto aanze kupewa uji ili kukidhi mahitaji maana mama yake anakuwa kazini! mnalazmisha watoto kukomaza utumbo mapema.

Ni wakati sasa sera zibadilike kunyonyesha ni miez sita na leave iwe miez 6, tulinde vizazi vyetu ili baadae wawe watoto bora wala sio bora watoto!
12 months itapendeza zaidi.
 
Haya yote yanatokana na wanaume wapumbavu wanaotaka kusaidiana maisha na wake zao, hadi kupelekea wake zao waanze kutafuta pesa hata katika mazingira ambayo yanafanya wasitimize majukumu yao ipasavyo, binafsi sitaki kusikia masuala ya mke wangu kuajiriwa ni either nimfungulie biashara au awe mama wa nyumbani nijue moja nimhudumie kila kitu ili atimize majukumu yake kikamilifu..
 
Kuna jinsi ya kuviweka katika hali ya usafi visipatwe na hayo unayoyasema na vinakuwa salama kabisa.
Kwa hali ya Wafanyakazi wengi wa Hii Tanzania unazani wana access sana na hilo?

Labda serikali ijenge sehemu za maternity kila ofisi, kitu ambacho ni kigumu .

Wapewe mwaka kabisa ,ila atleast mtu azae tena baada ya miaka mitatu toka amalize likizo ya uzazi...akiwai zaidi ya hapo ,akomae mwenyewe baada ya likizo fupi ya miezi mitatu.

Kwanza covid imetufundisha kuwa kufanyia kazi toka home inawezekana kwa kazi kadha wa kadha.
 
Kama unasema wapewe likizo ya mwaka ina maana hakutakuwa na hiyo likizo ya miezi mitatu, kama mtu atajifungua tena kabla ya huo muda apewe tena mwaka mzima wa kupumzika kitakuwa na ofisi hapo ndugu...?
 
Leave iwe mwaka, kwa manufaa ya watoto, imepita bila kupingwa
 
Hiyo itakuwa ni kazi au sehemu ya kupumzika ?
Yaani mimba ikifika miezi 7 tu mtu haonekani kazini, akishajifungua tena anakula miezi 3 na baada ya miezi 3 kuisha anakuwa anaingia kazini saa 2 na kutoka saa 6.

Kama anaona muda hautoshi achukue likizo bila malipo.
 
Malezi ya mtoto mchanga yanahitaji uangalizi mkubwa sana wa mama yake! Nashangaa serikali mnasisitiza mtoto asipewe maji wala uji ndani ya miez 6! yaani awe anashindia maziwa ya mama tu!

Nyinyi hao hao serikali mnawapa wafanyakaz wenu miez 3 tu ya materninty hamuoni tatizo kwa watoto kuwa badae wanakuwa na mapungufu mengi kwa kukosa malezi?

Miezi 3 maana yake mtoto aanze kupewa uji ili kukidhi mahitaji maana mama yake anakuwa kazini! mnalazmisha watoto kukomaza utumbo mapema.

Ni wakati sasa sera zibadilike kunyonyesha ni miez sita na leave iwe miez 6, tulinde vizazi vyetu ili baadae wawe watoto bora wala sio bora watoto!
Serikali pia iangalie, kama mzazi akipewa muda mrefu wa "maternity leave" basi alazimike kukaa muda mrefu bila ya kujifungua mtoto mwingine.

Mathalani, mzazi amejifungua mtoto wake mwezi Januari mwaka 2025, endapo atapewa mapumziko ya malezi ya kichanga kwa miezi 6, basi itampasa kuja kuzaa tena mtoto mwingine mwaka 2030.

Wale wanao totoa kila mara kama kuku, basi itakula kwao. Ni gharama kubwa kwa taasisi ama kampuni kuwa na mtumishi anaye jifungua mara kwa mara, na katika vipindi vifupi vifupi, na kutokana na upotevu wa muda mrefu uliotengwa kwa ajili ya malezi ya mtoto ama watoto wake.
 
Ni kweli lakn wafnyakaz wachache bado nyie mkicheleweshw huduma mnalia vumilien kwa iyi miez mitatu ni ming mkiendlea na kelele itwekw miwil
 
Serikali pia iangalie, kama mzazi akipewa muda mrefu wa "maternity leave" basi alazimike kukaa muda mrefu bila ya kujifungua mtoto mwingine.

Mathalani, mzazi amejifungua mtoto wake mwezi Januari mwaka 2025, endapo atapewa mapumziko ya malezi ya kichanga kwa miezi 6, basi itampasa kuja kuzaa tena mtoto mwingine mwaka 2030.

Wale wanao totoa kila mara kama kuku, basi itakula kwao. Ni gharama kubwa kwa taasisi ama kampuni kuwa na mtumishi anaye jifungua mara kwa mara, na katika vipindi vifupi vifupi, na kutokana na upotevu wa muda mrefu uliotengwa kwa ajili ya malezi ya mtoto ama watoto wake.
Kwa kawaida Maternity leave ni kila baada ya miaka 2 ya uzazi ukizaa ten kabla ya miaka 2 ya kujifungua unapata maternity leave ya mwezi 1 tu badala ya miezi 3 .
Unakosa baadhi ya haki zako za msingi itoshe kusema watu wapunguze kuzaa kwa haraka haraka
 
Hiyo Sheria ikipitishwa Zanzibar hakuna mwanamke ataenda kazini labda awe amefika menopause
 
Back
Top Bottom