comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Katika kuwatambua kisheria wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga nchini, Serikali inapaswa kuwabaini, kuwasajili katika mfumo sahihi wa kodi hivyo kupelekea wamachinga kulimbikiziwa kodi na kusumbuliwa na mgambo katika majiji, manispaa na maeneo mengine wanavunjiwa maeneo kuhamishwa na kuabdilishiwa maeneo ya kufanyia biashara kama hivyo ni bora wakarasimishwa kwa mtindo wa kisheria.
Aidha serikali inapaswa kutoa vitambulisho maalumu kwa wamachinga wote nchini ili kuzuia ukwepaji wa makusudi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa kati na wakubwa wakati wanawabinya wamachinga, wafanyabiashara huwatumia wamachinga kuwafanyia biashara na kuwalipa posho kidogo, vilevile kwa wale wamachinga wanaojitegemea nao hawajulikani katika mfumo maalumu wa kodi ya biashara serikalini.
Aidha umeibuka mtindo wa baadhi ya wafanyabiashara wa Kichina kujihusisha na umachinga kinyume na usajili wa baishara zao hali inayopelekea kukwepa kodi mara kadhaa