Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kama wewe umewahi kununua ardhi/kiwanja na kufuatilia hati ya umiliki katika ofisi za kanda,basi unaweza kuwa ni mmoja wa watu waliokumbwa na adha ya kutoka mkoa mmoja na kwenda mkoa mwingine ambako kuna ofisi za kanda kufuatilia hati yako na kukumbana na kero ya aina hii.
Moja ya matatzo au usumbufu ni mtu kufika katika ofisa usiku kufuatilia hati ya kiwanja chake na kuambiwa njoo tena siku nyingine kwasababu hati yako ilikuwa na mapungufu kadhaa hivyo haijafanyiwa kazi au kuambiwa njoo siku nyingine kwasababu hati yako bado haijakamilika kama tulivyokuahidi na sababu nyingine nyingi tu ambazo hutolewa na wahusika.
Kwa mfano,mtu huweza kutoka Singida au Morogoro kuja Ofisi ya kanda Dodoma kufuatilia hati yake na anapofika anaweza kuambiwa hati yako bado hivyo tunakuomba uje kesho au siku nyingine watakayokupangia.
Pia,hata kama wewe ni mkazi wa mkoa husika ambako kuna Ofisi ya kanda ya Msajili wa Hati, bado ni usumbufu kutoka unakoishi au kutoka kazini na kufika kwenye ofisi zao na kuambiwa hati yako bado haijakamilika kutokana na sababu kadhaa kama vile nyaraka kuandaliwa kimakosa baada ya mauziano ya hati au baadhi ya taarifa fulani kutokaa sawa katika rasimu ya hati yako,n.k na kuambiwa njoo siku nyingine na hivyo unakuwa umepoteza muda wako bure.
Hivyo,ili kuondoa matatzo ya aina hii na mengine yanayoweza kujitokeza kutokana na sababu mbalimbali na ili kumuondolea usumbufu mwananchi,nashauri serikali ibuni huduma ya hati mtandao kwa wenye access na mtandao wa internet na huduma ya hati mobile kwa wenye simu za mkononi(hata zile za tochi).
Kupitia huduma hizi,mwananchi huko aliko bila kufunga safari awe na uwezo wa kuingia online na kujua status ya hati yake(kama imekamilka,haijakamilika,kuna information zinahitajika au kuna marekebisho ya kufanya,n.k) ili hata mtu anaposafiri basi kwenda kuchuka hati yake asafiri akijua hali(staus) ya hati yake kama imekamilka au kuna nyaraka anatakiwa aziwasilishe upya,n.k kuliko hii ya mtu kwenda hujui hili wala lile na kufika na kuambiwa hati yako haijakamilika kwasababu hii au ile.
Na kupita huduma hiii,serikali inaweza kutoza gharama ndogo kwa kutumia huduma hii na hela zinazopatikana zinaweza kutumika kuendesha huduma hii na pia kikawa ni chanzo kimojawapo cha mapato kwa serikali kama ilivyo kwa makampuni ya simu na hata mabenki.
Najua kuna watu wasema huku ni kumuongezea mwananchi gharama, ila tujiulize, gharama kubwa ni ipi ya kuchajiwa vijisenti kidogo kwa kutumia huduma hii iwapo itaanzishwa au kusafiri kutoka sehemu ulipo na kufika Ofisi ya Msajili wa Hati na kuambiwa hati yako bado?
Na kwakuwa mwananchi huambiwa njoo siku fulani kuchukua hati yako,ni vizuri kwa mwananchi husika kutumia huduma hii kujua hati yake imefikia wapi baada ya muda alioahidiwa kutimia ili kama bado, basi asihangaike kusafiri kuchukua hati ambayo haijakamilika na hivyo kupoteza fedha na muda wake bure.
Faida nyingine ya kuwa na huduma kama hii, ni kumuwezesha mwananchi kujua mapema kama hati yake imekwama ili aweze kufanya anachotakiwa kufanya au kufuatilia mapema kunakohusika kuliko kusubiri siku ulioambiwa urudi kuchukua hati na kukuta kuna tatizo na ndio uanze kufuatilia.
Iwapo wazo hili litaonekana linafaa,basi wahusika wakae chini na wataalamu wa mambo ya IT na wa makampuni ya simu na kubuni huduma hii( mfano menu yake i-contain taarifa gani,n.k) kwani wao ndio wanajua zaidi.
Jambo lingine,kwasababu hati ni document nyeti na inapaswa kuchukuliwa na mmiliki halali wa hati hiyo au kwa kufuata taratibu zilizopo ikiwa anaechukua hati ni mtu mwingine tofautri na mmiliki halali wa hati husika,nashauri mtui anapowasilisha rasimu ya hati ili isajiliwe au mtu anaeleta hati ili ibadilishwe umiliki baada ya mauziano,mtu huyo(mwananchi) apewe namba maalumu ya siri atakayoitumia kama password kuingia katika mtandao utakaoanzishwa ili kumuwezesha kufuatilia status ya hati yake.
Ni ushauri tu wahusika ili kuondoa usumbufu na watu kujazana katika hizi ofisi wakati baadhi yao hati za hazijakamilika au zinahitaji marekebisha kabla ya kusajiliwa au kubadilishawa umiliki.
Tusijisifu kuwa na mavyeti mengi kama hatuwezi kuwa wabunifu na kutumia elimu zetu kusaidia wananchi wa kawaida kuondokana na shida au changamoto zinazowakabili/wanazokumbana nazo.