SoC03 Serikali ianzishe kazi huru mtandaoni kwa wahitimu elimu ya juu ili kutengeneza ajira na kuongeza ufanisi kwa waajiriwa serikalini

SoC03 Serikali ianzishe kazi huru mtandaoni kwa wahitimu elimu ya juu ili kutengeneza ajira na kuongeza ufanisi kwa waajiriwa serikalini

Stories of Change - 2023 Competition

Impimpi

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2019
Posts
466
Reaction score
964
Ni ukweli usiopingika kuwa mabadiliko ya kiteknolojia na sayansi hayana budi kutokea katika nchi yetu kama ambavyo ulimwengu mzima unashuhudia katika dunia ya sasa.

Hivyo, suala la Ajira za serikali na sekta binafsi limekuwa na ugumu wake licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali yetu kukabiliana nalo. Hata hivyo, ajira hizi chache zinazojitokeza haziwezi kukidhi mahitaji ya wahitimu wotewanaomaliza kutoka vyuo vya kati na vikuu. Katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia katika zama hizi za mapinduzi ya kidijitali na intaneti imekuwa rahisi kufanya kazi sehemu yoyote ile ili mradi tu mtu anao ujuzi wa kazi husika.

Wote ni mashahidi kuwa kipindi cha mlipuko wa UVIKO 19 mwaka 2020 watu wengi waliweza kufanya kazi wakiwa nyumbani na kazi kufanyika kwa kiwango kikubwa, hii inadhihirisha kuwa mapinduzi ya kidijitali yana mchango mkubwa katika Maendeleo ya jamii ya sasa. Hivyo, basi dhana hii ya mapinduzi ya kidijitali na intaneti ndio msingi mkubwa wa mada yangu ninayoiwasilisha katika shindano hili.

Kazi huru mtandaoni ni nini?

Bila shaka baadhi yetu tumeshawahi kusikia kuwa kuna watu wanafanya kazi mtandaoni na kulipwa na wateja wao kupitia tovuti ya kazi husika mfano Fiver.com na Freelencing.com ambazo ni tovuti zinazowakutanisha waajiri na waajiriwa wa muda mfupi na mara tu anapomaliza kazi husika basi hupewa ujira wake.

Kwa kifupi kazi huru mtandaoni ni uwepo wa mfumo wezeshi mtandaoni unaowakutanisha waajiri na waajiriwa kwa kuorodhesha kazi na sifa husika za mwajiriwa na kimsingi mwajiriwa huyu anakuwa huru kufanya kazi zake mtandaoni kwani anakuwa hafungwi na mwajiri katika taratibu za kazi kama kuwepo muda wote kazini na nyingine zinafanazo na hizo. Hivyo, inakuwa rahisi kwake kufanya kazi kwa waajiri mbalimbali kwa muda tofauti.

Faida mojawapo ya mfumo huu ni kumfanya mwajiriwa huru mtandaoni kujiingizia kipato na pia kuwa na muda wa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii. Pia, kumuongezea umahiri katika fani yake kwani ushindani uliopo katika kazi hizi humfanya kuwa makini na mjuzi zaidi siku hadi siku ili kuvutia waajiri.

Kwanini Serikali ianzishe kazi huru mtandaoni?

Kwa muda mrefu sasa wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu utoaji wa huduma katika ofisi za umma nchini kuwa kuna urasimu mwingi na uzembe uliokithiri. Na zipo dhana kuwa mtu akishapata kazi serikalini basi ameshajihakikishia uwepo wa ajira yake iwe ametimiza majukumu yake au la.

Pia, uwepo wa kazi nyingi katika ofisi za umma zinazoshindwa kufanyika kwa wakati kwa sababu ya uhaba au upungufu wa watumishi ni sababu muhimu kwanini serikali ianzishe mfumo huu wa kazi huru mtandaoni.

Mchakato wa uanzishwaji uweje?

Serikali mwaka 2008 ilianzisha wakala wa huduma za ajira Tanzania (TaESA) iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ili kuwaunganisha watafuta ajira na waajiri mbalimbali nchini.

Taasisi hii inaweza kuanzisha kitengo cha kazi huru mtandaoni kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali mtandao kwa kuanzisha mfumo wa pamoja utakaotumika kusajili na kutoa ithibati kwa watakaofuzu kama watoa huduma huru mtandaoni Serikalini na kuwaunganisha na Taasisi, wizara, mamlaka, Halmashauri na Mashirika ya Umma.

Pia, uandaliwe mfumo wa kuwapima utendaji kazi wao kulingana na majukumu na kazi walizozifanya kwa usahihi ili iwe rahisi kwa Taasisi za Serikali kutoa kazi kwa mtu aliye na ujuzi na uzoefu katika kazi mtandao. Wale watakaosajiliwa na kutambulika wapewe leseni na akaunti mtandaoni zilizo na mrejesho wa ufanisi wa kazi zilizofanywa na mtu husika.

Faida za Serikali kuanzisha kazi huru mtandaoni kwa wahitimu elimu ya juu ni pamoja na zifuatazo;
Moja, ni kuongeza ufanisi serikalini kwa kutoa huduma bora kwa wakati kwani mara nyingi huwa inaripotiwa kuwa uhaba wa wafanyakazi ndio husababisha kutotoa huduma kwa wakati hivyo endapo mpango huu utafanikiwa, utafanya kazi zifanyike kwa wepesi na tija.

Itapunguza uhaba wa ajira kwa vijana wahitimu wa vyuo Vikuu kwani watakuwa na uwezo wa kufanya kazi hizi kwa muda na kupunguza ombwe la uhaba wa Ajira.

Pia, mpango huu utaongeza uwajibikaji na ufanisi kwa watumishi wa serikali pia ujuzi na umahiri kwa vijana wahitimu wa vyuo nchini kwani ushindani utakuwa mkubwa.

Mpango huu utachochea matumizi ya intaneti yenye tija kwa vijana tofauti na hivi sasa ambapo mitandao inatumia kuharibu maadili ya Kitanzania hivyo vijana watapambana kutumia mitandao katika matumizi sahihi ili kujipatia kipato halali.

Na, mwisho vijana watakuwa wazalendo kwa Taifa lao kwani uwajibikaji na uzalendo ni kama mapacha.
 
Upvote 4
karibuni wadau kwa mawazo na mapendekezo zaidi
 
kura zenu ndugu zangu ni muhimu
 
Back
Top Bottom