Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba na serikali kwa ujumla msiwaonee huruma Watanzania.
Wengi wamezoea kuishi kwa madili na wizi.
Serikali inapoteza kiasi kikubwa cha fedha kwakuwa watu wanaikwepa. Kuna rafiki yangu ana biashara kwa siku faida ni 200,000 lakini kwa mwaka alikuwa analipa sh. 20000 ya kitambulisho cha machinga tu na sasa halipi hata Senti.
Kuna muda nilikuwa na duka karibu na TAZARA, nilishangaa kuona wafanyabiashara wenzangu kufunga maduka yao pindi waliposikia TRA wanakuja mitaa yetu.
Bodaboda hawalipi kodi huku mauzo yao kwa siku yanafika sh 30000, hata leseni wengi hawana ambazo zingesaidia kulipia kodi kila baada ya miaka 5 angalau. Mwisho wa siku wanaishia kuwapa pesa polisi na migambo. Tena ni pesa nyingi zaidi.