The Alchemist I
Member
- Jan 27, 2018
- 52
- 70
Dhana ya elimu na ajira kwa wahitimu
Wahitimu na fursa za ajira mbadala (Kujiajiri)
Nini kifanyike kuwawezesha vijana kujiajiri baada ya kuhitimu?
Matunda ya mpango huu kwa Jamii na Serikali
Ndoto kuu ya wazazi wengi katika jamii ni kuona watoto wao wakifanikiwa katika kila walifanyalo, kama ni biashara basi iwe yenye faida na kama ni elimu basi iwe yenye tija katika kubadilisha maisha ya watoto wao na hata yao wenyewe maana hiyo ndiyo dhana iliyo kuwepo kwa miaka mingi “mwanangu soma uje utusaidie”. Hata hivyo dhana hii ilikuwa ya kweli kwa miaka ya nyuma na wapo walio nufaika nayo ambao wengi wao ndio wazazi wetu leo.
Kwa miaka ya hivi karibuni jamii imeshuhudia mambo tofauti kidogo kulingana na dhana ya iliyo jengeka miongoni mwao, soko la ajira limekuwa changamoto kwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu huku wengi wa wahitimu hao wakijikuta wanapoteza dira na ndoto za maisha yao ya kesho kwa kushindwa kujisimamia au kujitegemea kwa wakati walio kusudia. Wengi wao wanajikuta wakiishi makwao na kwa ndugu wakiwa hawana wanacho fanya kiasi cha kuonekana mizigo, wavivu, wajinga au wasio jitambua ukilinganisha na vijana wa zamani (wazee wetu).
Kwa muda sasa suala hili limekuwa changamoto isiyo zoeleka katika jamii zetu na linachukuliwa kwa mtazamo na hisia tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine katika jamii. Kwa wastani, madai mengi yana ilenga Serikali moja kwa moja kwamba imeshindwa kushughulikia changamoto hiyo kwa kuto waajiri vijana kama ilivyo dhana ya elimu yetu nchini “baada ya kumaliza masomo ni kupata kazi”. Changamoto hii inapelekea vijana wengi kukata tamaa na kupoteza ndoto na malengo yao waliyo jiwekea ilihali wao ndo walipaswa kuwa nguvu kazi ya Taifa katika nyanja mbali mbali za uzalishaji na usimamizi wa rasrimali za nchi.

Katika nchi zinazo endelea kama Tanzania, zipo fursa nyingio sana za kibiashara kwa vijana wenye utayari na nyenzo za kutumia fursa hizo. Kilimo na ufugaji ni baadhi tu ya fursa za wazi ambazo kama zikichagizwa na elimu, utayari na nguvu kazi ya vijana basi kunakuwa na matokeo chanya zaidi yenye manufaa kwa vijana wenyewe, jamii na hata Taifa kwa ujumla kupitia tozo na ushuru katika mauzo ya bidhaa zitokanazo na kujiajiri. Hata hivyo mbali na uwepo wa fursa nyingi za kujiajiri, changamoto kubwa inayo wakwamisha vijana wengi kujiajiri ni msingi wa kuanzia.
Serikali inafahamu wastani wa uchumi wa familia nyingi za kitanzania, nyingi zina uwezo wa kati na chini na utakuta hata watoto wao wamesoma kwa michango ya ndugu wengi pamoja na kudra za Mwenyezi Mungu. Hivyo mara nyingi msaada wa familia kwa kijana unakoma pindi tu kijana anapo hitimu masomo kwa imani kwamba sasa atapata ajira au pengine atatumia elimu yake kujisimamia na kutengeneza uchumi wake ili kesho awe mfadhili wa familia. Wakati haya yakiendelea, kijana nae mbali na kukosa ajira licha ya kutafuta sana, utakuta hana pia mtaji unao mtosha kujiajiri kulingana na fursa anazo ziona hata kama ni nje ya taaluma yake.

Mimi kama kijana mhitimu wa zamani na mhanga wa changamoto ya ajira nchini, ninaishauri Serikali kupitia Taasisi yake ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) pamoja na mfuko wa pensheni kwa wafanyakazi (NSSF), ianzishe mpango maalumu wa kutunza asilimia kadhaa ya pesa za kila mwanafunzi kutokea kwenye fedha zao za kujikimu (BOOM).
Mpango huu utatatua changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa vijana wengi wanao hitimu masomo na kuwawezesha kujiajiri badala ya kusubiri ajira ambazo zimekuwa chache na ngumu sana kwa miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na zamani. Hekima ya kuwasaidia vijana hawa kutunza akiba inatokana na tabia/utaratibu wa wanafunzi wengi kujisahau na kutumia vibaya pesa za kujikimu wanazo pewa bila kujiwekea akiba kwani wengi huamini kuwa watapata kazi na kuanzisha maisha pindi watakapo hitimu, matumaini ambayo hugeuka shubiri muda mfupi tu baada ya kumaliza masomo na mwishowe hujikuta wahanga wa kuomba kazi hata zisizo stahili kulingana na hadhi ya elimu yao.
Ili kuleta tija katika mpango huu, utekelezaji unapaswa kuzingatia 30% ya kila fedha ya kujikimu anayopewa mwanafunzi. Hii inamaana kwamba mwanafunzi atachangia 15% ya pesa yake na Serikali imwongezee 15% kufanya jumla ya 30%. Nyongeza hii inakuja kama sehemu ya mpango wa Serikali kuwawezesha vijana kujiajiri kwani ukosefu wa ajira unachangiwa pia na uhaba wa maeneo ya kazi, suala la Serikali yenyewe. Hivyo nyongeza hiyo itakuwa kielelezo cha uwajibikaji wa Serikali katika kuwasaidia vijana katika kujiinua na kujenga Taifa lao kwani wao (vijana) ndiyo wanapaswa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu. Kwa miaka mitatu ya masomo, kijana mmoja hupata fedha za kujikimu mara 14 (Boom 12 na Mafunzo kwa vitendo 2), yaani mara 5 kila mwaka kwa miaka miwili ya kwanza na mara 4 kwa mwaka wa mwisho, hii ni kwa wanao soma miaka mitatu. Hivyo ikiwa fedha ya kujikimu ni kuanzia Tsh 500,000/=, basi 30% ya fedha hiyo ni Tsh 150,000/= ambayo ataipata mara 14 kwa kipindi chote cha masomo na atakuwa amejikusanyia zaidi ya 2,100,000/=(milioni mbili na laki moja). Pesa hii atapatiwa baada ya kuhitimu masomo ili imfae kwa kujiajiri kwani inatosha ikiwa atakuwa na utayari kuanza maisha pasipo kutegemea ajira.

Ikiwa mpango huu utawekwa katika utekelezaji, matunda ya mpango huu tunaweza kuyaona miaka mitatu baada ya kuanza utekelezaji kuanza. Tutaweza kuwaona vijana wetu wakijiajiri na kujisimamia badala ya kuwa mzigo kwa familia na jamii na Serikali kwani hutumia gharama kubwa kuwasomesha. Sambamba na hayo, tutashuhudia ongezeko la pato la ndani la Serikali kupitia ukusanywaji wa kodi pamoja na mzunguko wa fedha ambao utatokana na ajira binafsi za vijana hao. Mafanikio kwa vijana ni mafanikio ya jamii inayo wazunguka. Vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa.
Upvote
5