SoC01 Serikali ianzishe mpango mkakati wa kutoa elimu yenye tija kwa wanafunzi. Kujiajiri...

SoC01 Serikali ianzishe mpango mkakati wa kutoa elimu yenye tija kwa wanafunzi. Kujiajiri...

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Hasa kumekuwa na wimbi kubwa la watu kutafuta ajira huku wengine wengi wakiambulia patupu
Pengine sababu inaweza kuwa tunasoma na kufundishwa kwamba tupate vyeti ili mwisho wa siku tuajiriwe na hivyo ndivyo akili zetu zilivyojipanga ili kuweza kuyaishi maisha ya ndoto zetu hapo baade na pengine hii inatokana na uchochezi wa wazazi na walimu kwamba soma ili uje kuajiriwa huenda na hii imetukaa sana akilini mwetu huku tusijue kwamba kuna namna nyingine ya kulishinda hili nayo ni kujiajiri na si vinginevyo

Hivyo elimu itolewe kwa kuzingatia soko la ajira na ushindani wa mataifa mengine kwakuwa tunatakiwa tutambue na kujua njia sahihi ya kuweza kuyafikia mafanikio, Hivyo kama tatizo la elimu yetu kutokuwa bora basi ni kwamba mitaala ifanyiwe marekebisho kwa sababu tunataka elimu iwe na tija ili tuweze kuajiri wazawa kutoka ndani ya nchi yetu na sio kuruhusu nafasi zetu zichukuliwe na wapita njia ambao ni raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni hali hii itachochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa letu lote kwa ujumla
Hivyo mitaala iboreshwe ili kuhakikisha elimu yetu inazalisha wataalam wakubwa. Ambao watatusaidia katika kulijenga taifa.
Tukumbuke ya kwamba elimu bora ni msingi wa taifa lolote lenye nia ya kuendelea na kujikwamua kutoka kwenye dimbwi la umaskini

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Upvote 0
Back
Top Bottom