mackj
Member
- Jul 25, 2023
- 84
- 98
Kilimo cha maji (AQUACULTURE) ni sekta muhimu na inayokua kwa kasi zaidi ya uzalishaji wa chakula cha wanyama duniani, na inaendelea kuzidi kasi ukuaji wa idadi ya watu, huku usambazaji wa kila mtu kutoka kwa wafugaji wa samaki ukiongezeka kutoka kilo 0.7 mwaka 1970 hadi kilo 7.8 mwaka 2008, hii ikiwa ni sawa na ukuaji wa wastani wa asilimia 6.6 kwa mwaka.
Tayari imeshinda uvuvi wa kuvua kama chanzo kikuu Cha samaki wa chakula, Wakati uzalishaji wa ufugaji wa samaki (bila kujumuisha mimea ya majini) ulikuwa chini ya tani milioni 1 kwa mwaka mwanzoni mwa miaka ya 1950, uzalishaji kwa mwaka 2008 ulikuwa tani milioni 52.5, sawa na thamani ya dola za Marekani zipatazo bilioni 98.4 hii ni kwa mujibu repoti ya shirika la chakula duniani FAO ya mwaka 2010.
Kwa Tanzania robo ya wakazi wake wanategemea rasilimali za pwani au maziwa ya bara kwa ajili ya maisha yao. Zaidi ya watu 180,000 wameajiriwa katika sekta ya uvuvi, na watu wengine 19,000 wanajihusisha na ufugaji wa samaki.
Uzalishaji wa sasa wa samaki ni takriban tani 376,000 kwa mwaka, na karibu asilimia 97 ya samaki wanaopatikana kutoka kwa wavuvi wadogo na waliosalia kutoka kwa uvuvi wa biashara wakubwa. Kilimo cha majini kinazalisha tani 10,317 za ziada zikiwemo mwani (tani 450) na licha ya uwezo wake mkubwa, kwa kiasi kikubwa hazijatumika. Kwa sasa kuna mabwawa 21,300 ya samaki yanayotumika kwa ufugaji wa samaki.
Licha ya ulaji mdogo wa samaki nchini, kwa kilo 5.6/mtu/mwaka, samaki ni asilimia 19.7 ya ulaji wa protini ya wanyama nchini.
Takwimu hizi nikwa mujibu wa (world fish centre)
Misri ni nchi kubwa zaidi barani Afrika inayozalisha ufugaji wa samaki wa karibu tani 700,000 mwaka , Nchi nyingine muhimu barani Afrika ni Nigeria inayozalisha tani 153,000 za samaki wa kufugwa kwa mwaka Zambia tani 8,505, mwaka Ghana tani 7,154 mwaka na Zimbabwe (tani 2,652 mwaka takwimu hizi zilifanyika kwa nchi hizi mwaka 2009.
Mwaka wa 2008, mauzo ya nje ya samaki na mazao ya uvuvi duniani yalifikia rekodi ya Dola za Marekani bilioni 102, hadi asilimia 9 mwaka 2007. Licha ya kushuka kwa bei mwaka 2009 (wakati bei za vyakula zilipanda), data za shirika la chakula duniania FAO za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa biashara ya samaki imerejea - na utabiri wa muda mrefu unabaki kuwa chanya, huku sehemu kubwa ya samaki ikiongezeka uzalishaji unaoingia katika masoko ya kimataifa.
Mwelekeo unaoonekana katika takwimu hizi kwa ujumla ni kupanda kwa hisa ya jumla ya biashara kutoka kwa wauzaji nje, hasa kwa nchi zinazoendelea.
kwa sasa nchi kama zambia na zimbabwe ukiacha Nigeria na Misri zimepiga hatua sana katika sekta hii ya kikimo cha samaki kwa kuwa serikali za nchi hizo zimewekeza kwa wakulima wao kwa kuweka mifumo thabiti ya utoaji ruzuku ya chakula cha samaki na
utafiti wa mbegu bora
Kwa Kuanzisha vituo vya utafiti na kuwajengea uwezo wakulima kuwapeleka nchi zilizofanikiwa kama vile misri Nigeria pamoja na ghana kujifunza na kupata maarifa zaidi ili kuhakikisha wakulima wanafuga katika tija na kulipa kodi ya nchi na kuongeza pato la taifa lakini pia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupunguza tatizo la ajira.
Tanzania ni nchi yenye maziwa makubwa zaidi ya Matatu ukiachilia mbali madogo madogo pamoja mito, ambayo ni victoria, tanganyika, nyasa na rukwa na tumebahatika kuwa na bahari kubwa iliyoko katika mikoa zaidi ya mitatu ambako shughuli za uvuvi zinafanyika,
lakini pamoja na nehema hiyo aliyotupa mwenyezi Mungu bado rasirimali samaki haitoshelezi kutokana ukweli kwamba idadi ya watu imeongezeka kwa kiasi kikubwa na uhitaji wa samaki umekuwa mkubwa kwa mahitaji ya kitoweo na kibiashara hivyo kila mtu anategemea ziwa na bahari kupata samaki hivyo kufanya samaki kuendelea kupungua na kutokutosheleza huku uvuvi haramu na mabadiliko ya tabia nchi navyo vikitajwa kuwa chanzo kikuu cha kufanya samaki kutoweka
Ili kunusuru hali hii na kupata tanzania tutakayo yenye ushindani wa uzalishaji wa samaki bora na masoko ya uhakika na kupelekea sekta ya uvuvi kuwa mkombozi kwa uchumi wa nchi na ustawi wa mwanchi mmoja mmoja, ni kuwekeza katika kilimo cha samaki kama ilivyo kwenye kilimo cha mazao ya chakula na biashara hapa nchini,kwa kufanya yafuatayo:
1. kuanzisha mfumo wa ruzuku ya chakula bora cha samaki na uzalishaji wa mbegu bora kupitia mfumo wa vyama vya wafugaji vya msingi vya kila wilaya na mikoa ili kuvutia watu wengi kufuga samaki na kuacha kutegemea ziwa au bahari,
2.uanzishwaji wa vituo vya utafiti na uzalishaji wa mbegu bora za vifaranga wa samaki ili kuhakikisha wakulima wanapata uhakika wa mbegu bora, na uhakika wa matokeo chanya baada ya uvunaji
3.kuanzisha baraza la wataalum washauri wa kilimo cha samaki litakalo kuwa na wajibu wa kufuatilia na kuratibu masuala ya mafunzo na uzalishaji kupitia vyama vya msingi vya wakulima ili kutoa mbinu bora ya uzalishaji na kupanua wigo wa uzalishaji na masoko ndani na nje nchi kwa kuziongezea thamani samaki baada ya mavuno katika dhana ya usindikaji ili kuongeza tija kitu kitachofanya samaki au mazao ya wakulima kuanza kupanda thamani katika soko la kimataifa
4.kuwepo na wakala wa serikali wa uhakiki wa chakula cha samaki ili kutoruhusu chakula kisichofaa au chenye viini lishe hasi kwa matumizi ya samaki kitu kinachoweza kushusha thamani ya mazao ya wakulima pale yanapofika nje ya nchi kwa walaji wa mwisho
5.Kuwatambua wakulima na kuwasajili ili kuwapa namba za uthibitisho ili kuwafanya kutambulika kwa jumuiya zingine za wafugaji na mashirika ya kimaifa yanayohusiana na ufugaji samaki kama vile world fish centre n.k.
Pamoja na kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kudhibiti uvuvi haramu na kuboresha sheria na sera mbalimbali ili kudhibiti hali hiyo na kulinda rasilimali zitokazo na uvuvi lakini imesahau kuwa kila mtu anategemea ziwa na bahari, kwa kuzingatia mawazo haya itawabadilisha wananchi fikra kuwa siyo lazima ziwa au bahari ndio utatajirika au kupata fedha kutokana na uvuvi bali hata kwenye ufugaji samaki vinapatikana, hivyo watageukia katika ufugaji na baada ya muda mchache maziwa na bahari kama vyanzo vya asili vitarejea samaki kwa kiwango chake cha awali kwa faida ya kizazi kijacho na mazalia ya samaki yataimarika tena.
Naomba kuwasilisha

Attachments
Upvote
3