Librarian 105
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 261
- 356
Mfumo wa soko la ndani wa mazao na bidhaa za kilimo (na uvuvi) kwa kiasi kikubwa unaendeleza dhulma na unyonyaji kwa wazalishaji mali hizo. Ijapokuwa zipo jitihada za serikali zenye kukusudia kuleta ustawi wa sekta ya kilimo na uvuvi nchini, pia hapana budi hatua za haraka kuchukuliwa za kutathmini kisha kuyalinda maslahi na mitaji ya kifedha ya wadau wote muhimu kwenye sekta hii, na kwa munasaba huo andiko hili litajikita katika kuishauri serikali juu ya kuanzisha taasisi itakayodhibiti sekta hii kama ilivyo upande wa huduma za nishati na maji kunakosimamiwa na EWURA. Na uzito wa hoja hii unachagizwa na ukweli kwamba sekta ya kilimo (na uvuvi) unagusa unyeti wa usalama wa chakula, amani na utulivu, na vilevile kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Wakulima wengi hivi sasa hufikia hatua ya kuuza mazao yao mashambani kwa bei ya chini na kama haitoshi kwa kuzidisha ujazo wa kipimo cha gunia "rumbesa" kunakosababishwa na umaskini unaowakabili pamoja na njia za masoko ya bidhaa zao kuhodhiwa na madalali wanaoshirikiana na wafanyabiashara. Changamoto nyingine ni bei ya kununulia mazao yao wakati wa mavuno hushuka hata kutoendana na thamani ya mitaji na gharama zingine walizoziwekeza kwenye kilimo. Halikadhalika, kwa upande mwingine, soko kwa sekta ya kilimo limekuwa wazi mno kwa wageni kufuata mazao ya kilimo mashambani kabla na hata baada ya mavuno kulikopaswa kuzingatiwa kwa kanuni na sheria za forodha.
Hivyo basi, nukta kuu za andiko hili, ni muhimu zikapewa kipaumbele yaani a) udhibiti wa masuala yote ya huduma za ugani na, b) udurusu wa bei na kipimo cha mzani wa bidhaa hizo za ugani.
A) Udhibiti wa masuala yote ya huduma za ugani :
Chombo pendekezwa kitasimamia ubora wa bidhaa za ugani, usajili na taratibu za masoko unaoakisi kanuni za mahitaji na ugavi, kuweka miongozo ya uuzaji na manunuzi. Kwa ujumla eneo hili lilenge kuwaponya wakulima dhidi ya hila za madalali kuyazuia mazao yao muda mrefu au kuyatia kasoro za ubora ili kutengeneza mazingira ya kujinufaisha kiuchumi bila kuvuja jasho. Hivyo uratibu wa chombo hicho au taasisi hiyo unatakiwa uje kuondoa ukiritimba na uhodhi wa masoko ya mazao ya kilimo na uvuvi ili kufanya sekta hii ijiendeshe kwa kutegemea nguvu ya soko. Ikionekana inafaa, nafasi ya madalali, wanaweza kusajiliwa na kupewa leseni na pia kuainishiwa viwango vya huduma watakazopaswa kuzitoza kwa asilimia ili kukuza wigo wa kodi na vyanzo vya mapato ya ndani kwa njia moja au nyingine.
B ) Udurusu wa bei na kipimo cha mzani wa bidhaa za ugani:
Kwa hivi sasa tunaona bei ya mazao mara nyingi inamlalia mkulima kutokana na udalali kuwa sera isiyo rasmi inayodhibiti mitaji na nguvu ya soko. Kwa upande wa kipimo, mazao hununuliwa au hutolewa mashambani kwa ujazo wa rumbesa, na pindi yakifika mijini ama masokoni huuzwa kwa kupitia mzani wa kilo. Na katika kukaguliwa madalali hutumia vyuma vyao maalumu kuchoma magunia ili kuchota sehemu ya mazao hayo. Walakini baadae hawarejeshi sehemu hiyo kwenye mali ya mkulima bali huweka kwenye ndoo au kutupia ndani ya gari. Hapa hapana budi kupitishwe kipimo cha mzani na bei ipangwe kwa kila kilo kuanzia mashambani hadi masokoni na minada ya mazao kwa kuzingatia gharama za ukulima hadi mavuno kutegemeana na kanda za kilimo. Hii itaondoa sio tu dhulma ya rumbesa, bali pia, italinda thamani ya mavuno ya mkulima na ama mvuvi kwa kufuta hila ya waangusha bei hawa hasahasa wakati wa mavuno. Halikadhalika itaweka wazi soko la mazao ya ugani na kuwa lenye kuzingatia misingi ya uchumi wa soko huria.
Mwisho.
Uanzishwaji wa chombo kitakachodhibiti na kudurusu bei za bidhaa za kilimo na uvuvi. Kutanyanyua pato la wakulima na wavuni na wakati huo huo kukuza sekta ya kilimo na uvuvi, hii itawapa nguvu ya kiuchumi wakulima na wavuvi kuwekeza zaidi na kuiondoshea serikali mzigo wa matumizi na uwezeshaji wa mikopo ya kusaidia wakulima ambayo kwa asilimia kubwa huwa inaishia kuitia hasara tu. Hakika maslahi ya mkulima/mvuvi yakilindwa vyema kwa njia ya udhibiti wa huduma za ugani na udurusu wa bei na kipimo cha mzani, uwezekano mkubwa upo wa serikali kusitisha hata utoaji wa stakabadhi za pembejeo za kilimo na kisha kuelekeza fungu hilo kwenye maeneo mengine ya kimkakati. Huku yenyewe ikibakia kuilea sekta hii kama mdhibiti wa kisera na mwezeshaji wa mazingira ya kunufaisha na kulinda mitaji ya kifedha ya wadau wote wa sekta hii pasina kusahau kulinda haki za walaji wa mwisho.
Kuhusu muda wa utekelezaji wa mpango huu ni miaka mitano ; utakaoanza kwa wizara ya kilimo na uvuvi kukaa na washirika wake kuandaa sera, sheria, kanuni, na miongozo inayohitajika kuijenga taasisi imara iliyo huru kwa uwazi na uwajibikaji. Kisha serikali na bunge kuipa nguvu ya kisheria na kuiwezesha kibajeti. Ili kutimiza malengo ya mapinduzi ya kijani na kujenga uchumi jumuishi wa sekta ya kilimo na uvuvi nchini kukuza pato la taifa na njia za uzalishaji mali kijamii na kiviwanda. Kinyume chake, endapo serikali itaendelea kuwa mtoza ushuru na makato mengine kwenye sekta hii adhimu, wakulima na wavuvi watazidi kuogelea katika lindi la ufukara huku madalali na wafanyabiashara wakizidi kuneemeka kupitia jasho la wakulima na wavuvi.

Upvote
4