SoC04 Serikali iboreshe haya katika mfumo wa elimu

SoC04 Serikali iboreshe haya katika mfumo wa elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Aug 2, 2023
Posts
3
Reaction score
1
SEKTA YA ELIMU
"ELIMU" ni msingi katika maisha ya sasa naya baadae. napenda kuzungumzia kuhusu utoaji wa na ufaulishaji wa shule za serikali haswa za kata na nyinginezo. ili tuweze kuifikia tanzania tuitakayo ni lazima kubadili mfumo wa elimu kwa kuzingatia vitu vifuatavyo;

Mitihani ya kila wiki kwa ajili ya kujipima, shule nyingi sana takribani nchi nzima haswa maeneo ya vijijini hakuna utaratibu wa kuwapima wanafunzi katika moduli walizosoma au majaribio ya wiki hivyo kutokuweza kutambua uwezo wa wanafunzi husika. hivyo basi walimu wajue nini wanafanya ili kuongeza ufaulu zaidi.

Kumaliza moduli kwa wakati, katika shule nyingi za serikali wanafunzi wanashindwa kufaulu mitihani kwa sababu ya kutokusoma baadhi ya moduli muhimu. na walimu mara nyingi hupenda kufundisha zile mada nyepesi kwao na sio zote haswa kwa shule nyingi za vijijini. hivyo basi serikali iongeze bidii kuhimiza changamoto hiyo.

Kushughulikia matatizo ya wanafunzi, walimu wengi wamekuwa wavivu wa kusikiliza changamoto za wanafunzi hivyo kupelekea wanafunzi kukosa uwezo wa kujiamini na kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao na kusababisha kushindwa kufaulu katika mitihani yao. ningeomba serikali iweke dawati maalumu kwa ajili ya kusikiliza changamoto za wanafunzi shuleni.

Ukosefu wa maktaba na maabara mashuleni, serikakali inafanya juhudi kubwa kutoa vitabu na vifaa vya maabara mashuleni lakini badala ya kutumika kwa wanafunzi shule huvifungia vitabu na vifaa hivyo store kwa sababu ya ukosefu wa jengo maalumu kwa ajili ya kuhifadhia vitabu na vifaa vya maabara hivyo wanafunzi kushindwa kujisomea na kutokupata vitabu kwa wakati kwa sababu ya uvivu wa walimu kutoa vitabu store. hivyo tuamke ili tuweze kuendelea kielimu.

Uwepo wa makambi shuleni haswa kwa madarasa yenye mitihani, watoto kukaa kambi (boarding) za shuleni hapo kwa muda wa kipindi cha kukaribia mitihani inasaidia watoto kujisomea kipindi cha usiku na asubuhi na kuondokana na kero za nyumbani za wazazi. mfano shule ya msingi na sekondari za Norini Wilaya ya Kongwa zinautaratibu huo na tangu uanzishwe shule zimekuwa zikiongezeka kitaaluma.

Mitihani ya kiwilaya na kimkoa, ili wanafunzi wafaulu vizuri na kuongezeka kitaaluma ni muhimu serikali kutunga mitihani ya kiwilaya na kimkoa kila baada ya miezi miwili kwa kuzingatia muundo wa mtihani wa taifa ili kumuondolea mwanafunzi uoga wa mitihani ya kiwilaya au mkoa na itamuwezesha kujiendeleza vema. sio lazima kutolewa nakala huko ofisini ila kutuma (softcopy) nakala ya mitihani hiyo kwa njia ya internet na shule itakuwa na wajibu wa kuprinti huko iliko na kuwapatia watoto mitihani hiyo.

Kazi za nyumbani na mazoezi ya kila siku, walimu wengi hawana utaratibu wa kuwapa kazi watoto pindi wanapomaliza kipindi cha siku au maswali ya moduli husika, hivyo inapelekea mwalimu kutokelewa kuwa mtoto ameelewa moduli au kipindi alichofundishwa ili aweze kutatua changamoto hiyo na kuwaelekeza vizuri.

Ukosefu wa madawati na madarasa, mwanafunzi ili aweze kuelewa vizuri kuhusiana na somo analofundishwa ni lazima awe katika hali nzuri ya kufundishiwa hivyo endapo serikali itajitahidi kutimiza madarasa na madawati kwa wakati ni matumaini yangu kuwa watoto karibia wote watafaulu kwa sababu akili zao zitakuwa haziwazi mkao au baridi au vumbi na mengineyo.

Kuzuia na kupinga dawa za kulevya, wanafunzi wengi wanajiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya hususani bangi na pombe kali haswa kwa wanafunzi kuanzia darasa la sita hadi kidato cha nne, na hii nimeweza kuithibisha katika kijiji cha Norini, Matongoro, Mlanje, Songambele na Mkoka wanafunzi kutoka katika vijiji hivi wamekuwa wakitumia madawa ya kulevya ingali bado wadogo na kusababisha kuacha shule na wengine kutokuzingatia masomo wawapo darasani. hivyo serikali ikiweka jitihada ya kukomesha madawa haya kwa sheria kali naamini kuwa elimu yetu itapanda viwango na tutafikia katika Tanzania tunayoitaka.

Veta kutoa vyeti kwa kila mtu,
masomo yanayotolewa na veta ni mazuri na yanaongeza ujuzi kwa wanafunzi na kwa nchi pia. lakini kumekuwa na tatizo la kutokutoa vyeti vya wanafunzi ambao wameshindwa kufaulu hata somo moja na kusababisha vijana hawa kushindwa kupata kazi zinazoendana na ujuzi wao kwa kutokuwamiwa kuwa wamefika na wamesoma chuo cha ufundi. hivyo basi endapo tukatambua kuwa vyeti hivi vinaumuhimu kwa vijana kupata ajira na kuachana na wizi, ukabaji na vyote vinavyoendana na uharifu na kupitia cheti akapata sehemu ya kuonyesha ujuzi wake hata kidogo.

Hitimisho, nchi yetu Tanzania inauwezo mkubwa sana wa kufanya mambo na yakatimia na ninaamini katika mambo yote hayo inaweza kufanya jambo. Lakini endapo ikazingatia mambo yote tajwa hapo juu nchi yetu itakuwa moja ya nchi zilizoendelea kielimu zaidi. mwisho nawasalimu kwa kusema Tanzania bila kufeli kunawezekana.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom