A
Anonymous
Guest
Habari!
Tunaomba serikali ya Wilaya, mkoa na hata Wizara inayohusika kuingilia kati sintofahamu iliyopo soko la matunda na mbogamboga Msufini - Singida, kati ya wajasiriamali na wenye eneo (chama)
Kumekuwa na sintofahamu kadhaa katika soko hili ikiwemo kukosekana kwa uwazi, hasa juu ya mabadiliko ya kimatumizi ya eneo hili ambapo kuna ujenzi wa vyumba vya biashara (fremu) unaendelea, lakini haifahamiki soko la mbogamboga na matunda litahamia wapi, lini na kwa utaratibu upi.
Tayari mchakato wa ujenzi huu umeshawaondoa wajasiriamali wasiopungua 30 eneo la mbogamboga kupisha ujenzi, pasi na kuwaelekeza eneo mbadala na hawajui cha kufanya kunusuru uchumi wa familia zao uliotegemea kazi zao.
Hali hii imeleta hofu kwa wafanyabishara na wajasiriamali kwa ujumla ambapo sio chama wala serikali, hakuna anayetolea ufafanuzi na kauli thabiti juu ya mstakabali wa wajasiriamali waliopo eneo hili
Tunaiomba serikali, kwa maslahi mapana ya wananchi wake ichukue hatua stahiki za ama kurasmisha eneo hili liwe soko la kudumu, au kutenga eneo jingine mbadala na rafiki kisha kuweka utaratibu mzuri wa kuwahamishia wajasiriamali. Tunashauri mbinu shirikishi itumike ili kurahisisha kazi na kuepuka urasimu.