Serikali ieleze mnunuzi wa korosho inalipia kiasi gani ili kupata bei halisi

Serikali ieleze mnunuzi wa korosho inalipia kiasi gani ili kupata bei halisi

chikambabatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
1,339
Reaction score
1,318
Katika hali ya wakulima kulalamika juu ya bei ndogo ya kuuzia korosho, mkulima awekwe wazi kuwa kiasi kungine amelipia viatilifu, hili hesabu yake ikae sawa.

Mtindo wa kugawa viatilifu bure usirudiwe tena, kwa sababu haziendani na kiasi mkulima halisi anacholipia, pia ugawaji hauzingatii uzalishaji. Mkulima anazalisha tani tatu, amepewa lita tano za sulphur ya maji yenye thamani ya 70,000/=, iwapo mnunuzi ataondoa 100/= kila kilo, mkulima atapoteza 300,000/ bila kutoa ile 70k.

Wabunge walihoji juu ya kukatwa viatilifu kwa kila muuzaji wa korosho kwa kilo, walitaka achukuae alipie kiasi alichochukwa, serikali mkasitisha mpango huo ila mkauzungushia kwa nyuma, eti wanalipa wanunuzi, ili jambo baya sana.

Ndio pale Ndugai anasema mawaziri hawashauriki, katika ili waziri wa kilimo ushauriki!
 
Sielewi kabisa kwanini Serikali ina jihusisha na ununuzi wa korosho ( masoko yamejaa Google kila kona), na iache kudhulumu wakulima kwa mikodi msururu isiyo na maana yeyote zaidi ya kuua biashara za watu
Utakuta ma-dc wanavalia njuga zao la korosho utafikiri wanawaonea huruma wakulima, nao wanaweka makato yao, eti kila kilo kiasi fulani tuchangie timu yetu ya mipira, pesa za mpira toka makato ya korosho haziko wazi, sijui anakagua nani ni uonevu tu!
 
Hivi mbona mnasahau mapema sana jamani?

Tangu lini ccm iliwahi kuwajali wananchi kwenye shida zao kwa dhati?
 
Poleni sana wakulima wa kusini kote ningewashauri mgekuwa na utaratibu wa kuwatembelea wakulima wa kaskazini mkaona jinsi wanavyo ikatalia serekale kwenye mbinu zake za kuwanyoonya.
 
Hivi mbona mnasahau mapema sana jamani?

Tangu lini ccm iliwahi kuwajali wananchi kwenye shida zao kwa dhati?
Wasijali tu ila wasitunyang'anye hela zetu, kutuuzia lita sulphur zaidi la laki wakati haizidi elfu kumi na tano!
 
Back
Top Bottom