MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hili suala la ukosefu wa ajira ni tatizo la dunia nzima ila hatupaswi kubweteka kisa majirani nao wana tatizo kama letu. Kama mwananchi mzalendo nina ushauri kwa serikali ili kupunguza tatizo la ajira lililopo na kuzuia huu uanzishwaji wa vikundi vya vijana wasio na ajira.
Haileti picha nzuri vijana kuunda umoja wa wasio na ajira. Binafsi naona haijakaa poa kwa amani yetu tunayoilinda kwa wivu mkubwa.
Ninashauri serikali iwapige jeki vijana wote wa fani mbalimbali walioanza kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili nao waweze kuwaajiri wenzao. Sio kila mtu anaweza kuongoza biashara ikakua. Kwa hiyo wale wanaoweza wawezeshwe ili wasaidie wengine.
Kuna vijana wako kwenye kilimo, IT, Mechanics, trading, hospitality, nk. Wakipatikana vijana 100 kila mkoa wanaofanya vizuri kwenye biashara zao wakakopeshwa Tsh 100m kila mmoja bila riba itasaidia sana kukuza mitaji yao hali itakayolazimisha kuajiri vijana wenzao.