Tumchague Kagame kuwa Rais TZ. Ndani ya miaka 20 amefanya makubwa kwa Rwanda, akiwa Rais Tanzania ndani ya miaka mitano atafanya miujiza. Utani.
Kama kanchi kadogo hako kana tuuzia magari, kiwanda cha mobile phones, kakuza utalii, kaongeza elimu, afya, makazi kwa watu wake, technologia, mazingira mazuri ya biashara, uwekezaji, accomodation, usafi na usalama nchini kwake. Amezibiti urasimu, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma, (Tax regime) kodi zinazoeleweka, zenye uhalisia, zinazochochea ukuzaji wa biashara na uwekezaji.
Imagine angefanyaje na resources zote za Tanzania ilizonazo zaidi ya mara mia moja ukilinganisha na Rwanda.
Gas, utalii, fukwe, bandari, mazao, rasilimali watu, madini, samaki, mifugo, ardhi, strategic location (tumezungukwa na nchi nane), vyanzo vya maji, Amani na utulivu.
Tunahitaji visionary and serious leaders.