Serikali ifike wakati muwaonee huruma Watanzania wenzenu. Mtafanya propaganda za namna hii mpaka lini?

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Your browser is not able to display this video.

Itazame hii video halafu jiulize maswali 5 kisha uyatafutie majibu wewe mwenyewe.
Serikali inawajibu wa kutoa ajira kwa vijana wote.
Ajira kwenye taasisi za kiserikali.
Ajira kwenye sekta binafsi
Ajira binafsi (kujiajiri).

Iwe ajira za serikali, za sekta binafsi au za kujiajiri serikali haipaswi kukwepa jukumu lake katika kihakikisha ustawi wa vijana.

VETA wapelekeni kwanza vijana waliokosa elimu ya sekondari na wale walioishia kidato cha 4 na 6 ambao hawajabahatika kwenda chuo kwasababu za kiuchumu maana hao hawana fimbo mkononi .

Vijana wenye astashahada, stashahada na shahada tayari wana fimbo mkononi muwatengenezee mazingira yao tofauti na vijana wasio na fimbo mkononi.

Tukiwa na utaratibu wa kuchekea kila kitu baadaye kiongozi ataropoka kuwa baada ya VETA sasa vijana wachangamkie course ya safety and first aid OSHA au Zimamoto ambako nako watakamuliwa malaki kwa course ya wiki moja
 
Wauze hata kuku watu wanatoboa na vyeti vyaao kwa kazi zilizokuwa hazifanywi na wenye vyeti...kuna dogo hapa ana dip ya education amejifunza kuuza genge na mamake kaingia kuuza kuku sasa hivi ana noah mpya ya biashara na boda safi ya mishe zake...
 
Huku ni kupoteza muda. Kwanini hizo course za ustadi/ufundi, zisiingizwe kwenye shule za msingi na secondary? Mitaala yetu ya elimu ni duni saana
 

Matapeli hawa
 
Tuna viongozi wapuuzi walioshindwa kutekeleza majukumu Yao na kuleta sababu zisizo na msingi wowote.

Kuna Mass failure kidato Cha nne Kwa nini hao ndio iwe lazima kwenda VETA??

Degree zikienda VETA, Diploma VETA, Certificate VETA, form Six VETA, form four VETA na darasa la saba VETA baada ya miaka 10 tu HAKUTA KALIKA tutarudi kule kule tu.

Sera na sheria za Nchi inabidi zibadilishwe


1., toa passport Kwa vijana wote nchini

2. Weka sheria vijana wote kutoka kidato Cha nne waende VETA japo miaka 2

3. Toa mikopo nafuu Kwa makundi ya vijana 100 waliotoka VETA.

3. Punguza umri wa kustaafu kutoka 60 hadi 55.

4. Ondoka nafasi zote za uteuzi ziwe za ushindani.

5. Weka mazingira rafiki ya biashara

TATIZO SERIKALI YA CCM HAWAWEZI KUFANYA HAYO NI WAOGA NA INCOMPETENT...

Asante.
 
This is good
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…