SoC04 Serikali ifuatilie miamala ya kifedha kwenye taasisi za kidini zilizopo Tanzania

SoC04 Serikali ifuatilie miamala ya kifedha kwenye taasisi za kidini zilizopo Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

fundi radio

Member
Joined
Apr 2, 2023
Posts
52
Reaction score
95
Kumekuwepo Kwa taasisi nyingi za kidini zinazo Jenga majengo ya kuubadu na kufanya shughuli zao Bila serikali kujua upatikanaji wake na matumizi ya pesa za hayo mashirika ya kidini.

Kuna baadhi ya viongozi wa hizo taasisi wanaoneka wakiwatupia wananchi pesa, (kutoa / kumpa MTU pesa Sio kitu kibaya) Ila kutupa pesa barabarani na watu kukanyagana ili kupata Elf kumi, huu ni utovu wa nidhamu, wanaonyesha ufahari wa Mali zao Kwa waumini Wao ,ambao ni masikini wa kutupwa.

Je, hizo pesa wanazo zirusha wamezipata kupitia sadaka za waumini wao? Kama ni hivyo basi wanawakosea heshima waumini wao, na kama Sio ingependeza kutaja vyanzo vya utajiri wao, ili wawe kiigizo chema Kwa waumini wao.wajivunze maendeleo kupitia kwao.

Mwaka huu US Aid Tanzania, walitoa msaada wa chakula Kwa watoto wa mashuleni wa nyanda za Kati , ili kupambana na utapiamlo. Lakin ilitokea taasisi ya kidini ya hapa Nchi ikitoa kauli za kibaguzi na za uchochezi wa chuki dhidi ya USA aid Tanzania.

Sote tunajua USA aid Tanzania, ni pesa za walipakodi wa raia wa kimarekani Kwa ajili ya kusaidia mambo ya AFYA, Elimu, wanawake na maendeleo, nishati Safi, nk. Je hii taasisi ya kidini inayopinga misaada ya US Aid Tanzania, Wao pesa zao wanatoa wapi na Kwa kusudi Gani?, za kujenga nyumba za Ibada kila Kata.

Na kwanini wanafanya hivi ina maana watanzania mahitaji Yao ni nyumba za kuabudia tu. Mbona Wao hatuwaoni wakiwasaidia jamii ya kitanzania MOJA Kwa MOJA kupambana na umaskini, isipokuwa Wao msaada Wao ni kujenga nyumba za Ibada Tu, labda na visima, na unakuta kisima kinajengwa rufuji , ambapo panatokea mafuriko ya Mto.

Kinachotokea wanapandikiza chuki kwa hawa watu masikini juu ya serikali Yao namwishowe kuwa magaidi.
Haya hapa chini ni baadhi Tu ya masuluhusho!

1. Kufanya marekebisho ya Kisheria na Sera kuendena na wakati
Serikali ya Tanzania izifanyie marekebisho ya sheria na sera za kudhibiti utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji Fedha ya mwaka 2006, ambayo inatakiwa kurekebishwa ili kuendana na wakati uliopo Sasa, ili kuweza kutoa mwongozo wa mamlaka kwa taasisi za kifedha na zisizo za kifedha, ikiwemo taasisi za kidini, ili kuhakikisha kuwa hakuna shughuli haramu zinazofanyika kupitia mifumo yao.

2. Usimamizi na Ufuatiliaji wa Taasisi za Kidini
Serikali ianzishe mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa taasisi za kidini. Taasisi hizi zinatakiwa kusajiliwa rasmi na kutoa ripoti za kifedha zilizohakikiwa na mamlaka husika. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinahusika na kuhakikisha kuwa michango na matumizi ya fedha katika taasisi hizi yanakaguliwa mara kwa mara, na taarifa zao ziweze kupatikana Kwa umma kirahisi pindi Tu zinapo hitajika na waumini, wasomi, waandishi wa habari.

3. Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa
Tanzania ijiunge na mashirika mbalimbali ya kimataifa yanayopambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi kama vile Financial Action Task Force (FATF). Ushirikiano huu utasaidia kubadilishana taarifa za kiintelijensia na kupata msaada wa kiufundi katika kuboresha mifumo ya ndani ya udhibiti wa fedha haramu.

4. Kutoa Mafunzo na Uhamasishaji
Serikali iwekeze katika kutoa mafunzo kwa viongozi wa kidini na waumini juu ya athari za utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Kampeni za uhamasishaji zifanyike mara kwa mara ili kujenga ufahamu na uelewa wa umuhimu wa kuzuia fedha haramu kuingia katika taasisi za kidini.

5. Kuboresha Teknolojia na Mifumo ya Kielektroniki zisomane
Serikali ieanzishe mifumo ya kielektroniki ya ufuatiliaji wa miamala ya fedha. Mifumo hii itasaidia kufuatilia haraka na kwa ufanisi miamala yenye mashaka na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi wa kina.

6. Kuongeza Ushirikiano wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
Vyombo vya ulinzi na usalama kama vile Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa vina jukumu kubwa katika kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika wa utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Ushirikiano huu utahakikisha kuwa taarifa zinazopatikana kutoka kwa taasisi za kifedha na kidini zinachukuliwa hatua stahiki.

7. Kuimarisha Udhibiti wa Mipaka na Uhamiaji
Kudhibiti mipaka na shughuli za uhamiaji ni muhimu katika kuzuia mtiririko wa fedha haramu. Kuna raia Wana beba pesa kwenye mabegi huko mipakani. Serikali izidi kuimarisha udhibiti wa mipaka kwa kutumia teknolojia na kuimarisha ukaguzi wa wageni wanaoingia na kutoka nchini kwetu.

Hitimisho
Serikali Makini Hata siku moja haitegemei taasisi za kidini kuwa ni sehemu ya kutafuta ushawishi Kwa wananchi wake. Serikali inatakiwa ijue vipaumbele vyake, isitegemee kuna watu kutoka nje watakuja kutatua matatizo Yao.
 
Upvote 2
Dini ni siasa ya kale,na ni mkono wa kushoto wa utawala katika siasa za kisasa,huwezi sikua wanaingiliwa mipango yako mana wanasaidia watawala kutawala.
 
Huyo shekh kitendo cha kukubali kosa mapema, ni kiashiria Kwamba kuna maovu anayaficha.

- miamala ya malipo iliyofanywa na wazazi wa watoto hao kwa huyo shekh ichunguzwe yote kikamilifu.

- kupitia Nida wachunguze kila wazazi wa watoto hao, kuna possibility ya kuwepo wahamiaji haramu apo.

- watoto hao wachunguzwe afya zao, na kuwaangalia kama wamefanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Pia Bado kuna vikundi kama hivyo hapo pwani, Dar, ilala,kigamboni, Tanga, Kilimanjaro, Arusha,singida, kigoma , Lindi, mtwara 👈 Haya maeneo tajwa , kamati za usalama mkazifanyie Kazi kikamilifu,

Huyo shekh ana makosa mengi ya kisheria kayavunja, anatakiwa afikishwe kwenye vyombo vya usalama na kisheria kujibu maswali na mashitaka ya matendo aliyoyafanya.
 
Tamaduni za watu wa pwani ni za hovyo saana,


 
Kazi ni kipimo cha UTU VIONGOZI WA KIDINI WAJIBIKENI WAKATI TULIO SASA SIO ZAMANI.

 
Back
Top Bottom