VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Naiomba sana Serikali ya chama changu. Iheshimu suala hili nyeti la katiba mpya. Katiba ni moyo wa nchi. Si jambo la kuletewa mzaha na maigizo. Nimesikitishwa sana na nilichoshuhudia kuhusu nakala za Katiba Inayopendekezwa. Kimeniuma sana. Nimelia kuililia nchi yangu inayoelekea shimoni.
Nimeshuhudia nakala za katiba zikiwafikia wananchi. Nimeshuhudia wananchi wakisoma kwa zamu,kwa saa chache,halafu nakala hiyohiyo kuhamishwa kwenda nyumba nyingine. Nimeshuhudia Katiba Inayopendekezwa ikisomwa kama gazeti. Nikalia sana.
Nimesikitishwa na mtazamo wa Serikali kuwa wananchi wanatakiwa kuiona na kuisoma tu Katiba Inayopendekezwa. Si kuielewa ili kuchagua upande sahihi kwenye kura ya maoni. Huu ni mtazamo hasi na wenye ukakasi. Ni mtazamo wa kiutani,kisanii na kimaigizo. Katiba ni nyaraka ya kisheria. Hata wasomi wenyewe waweza kuisoma na wasielewe. Seuse wananchi wa kawaida?
Serikali,tafadhalini,muwe makini. Kucheza na Katiba ni kuchezea moyo wa Tanzania. Tujirekebishe na tustopishe hima!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam