Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Wanatumika kutakatisha Pesa.. hawawezi kuzuiliwa kamwe[emoji23][emoji23][emoji23] mpaka siku Akili zitakapo Wakaa Sawa
 
Serikali ndio hasa inapaswa kujitathmini kwa umasikini mbaya kabisa wa watu wake. Umasikini ni kama janga la mafuriko ya Hanang' ukikukumba ni lazima utahaha sana kujinasua, bado serikali inahitaji kuongeza nguvu katika kupambana na Maradhi, Ujinga na Umasikini.
 
Serikali ni kama Kanisa, inakamua wanyonge na kuwapa mafao matajiri.

Mchawi hawezi mkamata mchawi mwenzie!
 

Safi sana kwa ujumbe huu. Mimi kuna kanisa X Mkoani Dodoma wilaya X kila siku Mchungaji wake ananipigia simu niende kwenye maombi kila siku. Nishamkatalia Ujinga huo. Siku ya Jpili inatakiwa utoe Sadaka awamu 4 si ni kutiana umasikini. Watanzania tutaendelea kuwa masikini kisa kuamini maisha ya miujiza bila kufanya kazi kwa bidii.
 
Bora huko kwa manabii wananchi wanapeleka kwa hiyari yao hata wakifirisika wametaka wenyewe. Sasa CCM mnaiba hela za walalahoi kwa lazima bila hiyari yetu wananchi na mnakuwa mabilionea kwa wizi.
Kila mwaka ripoti ya CAG inaonesha wizi mkubwa wa mabilioni mnaofanya viongozi wa serikali ya CCM kwenye hela za walalahoi na hamuachi.
Wizi wa mabilioni Epa, Escrow, Atcl, kula kwa urefu wa kamba kwa kuteuliwa na rais etc etc.
Kabla ya kuwanyooshea vidole manabii wanyooshee vidole wateule wa CCM waache uporaji vinginenyo hao manabii hawawezi kuacha maana viongozi mafisadi hawafanywi chochote.
 
Pascal Mayalla mungu akubariki kwa kuyasema haya, una roho ya kipekee.

Wale watu wanaopeleka sadaka huko sio wajinga kama watu wanavowaita, hao watu wanaowaita wajinga ni kwasababu tuu maybe hawajawahi kushikwa na matatizo hadi wakakosa tumaini, kama ulipata matatizo na ukaya-solve bila kwenda kwa hao watu ni jambo la kumshukuru mungu kwa hekima uliyokuwa nayo, sio unaanza kuita watu wengine wajinga, they are just desperate, wamekumbwa na matatizo, majanga na umaskini unawasumbua imefika wakati sasa uwezo wao wa kufikiri umepungua, atafanya lolote ilimradi maumivu yaishe au aondokane na dhiki yake.

Ni vibaya sana na sio ubinadamu kutumia weakness za mtu anayehitaji msaada wako kumtapeli, kwa upande mm huwa inaniuma sana, hakika mungu anawaona na haki ya mungu itawafikiwa wanaofanya huo uhuni.

Na sio tuu hivo brother Pascal Mayalla huwa sometimes wakishamaliza kuwatapeli na kuwakomba hela zote wanawaua ili kupoteza ushahidi, inasikitisha sana kwamba wanatumia jina la mungu kufanya haya mambo bila hata aibu.

Nasikitika kusema kwamba serikali haiwez ingilia kati kwasababu hata serikali yenyew wanashirikiana nao, huwaita kweny mikutano yao ya kampeni za uchaguzi n.k
 
matatizo ya kiroho ni kweli yanawasumbua watu wengi na hii imesababishwa na watu kushindwa kuishi Cleanest Life style .

Hivyo serikali itoe tu Elimu sahihi Kwa watu wake kuhusu maswala ya kiroho utatuliwa na MTU mwemyewe na sio nabii then umasikini Wa uchumi ndo huwa unazalisha umasikini wa fikra.


Taifa linasumbuliwa na ujinga ,maradhi,umasikini na sasa NYEGE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…