Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

P unatafutwa huku popote ulipo fanya kama unajikuna uoneka tafadhali 🤔
 
Waumini wenyewe si ndio wanasemaga Israel ni Taifa teule la Mungu, so obviously sisi ni Taifa la Kishetani. No wonders
 
Mkuu peleka hii kule kwenye " Vituko mitandaoni, tupia chako".
Cc: Pascal Mayalla
 
Sio makanisa ya miujiza tu hata RC kuna michango balaa,mara kutegemeza jimbo au parokia,sherehe za somo wa jumuiya au kigango,michango ya gari la paroko, gharama za ndoa,malipo ya kukodi kwaya kwenye ibada ya ndoa,malipo ya ubatizo,kipaimara,kumunio.Nako pia kuna maji ya baraka,mafuta ya karisma.Tofauti yake manabii wana show za sole singer RC na wenzake wanafanya kolabo(Kitaasisi).
 

Ni kweli kabisa,kumeingia huu upepo wa ishara na miujiza pamoja na prophecy za uongo mtupu.actialy inaweza kuwa asilimia kubwa ya wanaojiita watumishi wa Mungu walitakiwa wasajili hiduma zao kwenye kategory ya tiba asili. yaani wapewe kibali sana na kile alicho nacho Dr.Manyau nyau
 
Kuhani Musa pale Kimara Temboni kaporomosha mjengo wa billion kadhaa! Alianzia kwenye banda la mabati!
Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.

Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.

Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.

Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.

P
 
Kuna kipindi nilifikiria kuwa hawa wa hubiri ni sehemu ya serikali wapo ili kuwa pumbaza wananchi ili wakubwa wa endelee na mambo yao
 
Bora RC,ni taasisi na utaona yale maendeleo ya kujenga makanisa .shule hospitali na kadhalika.ila hizi huduma binafsi kila kitu ni binafsi
 
Ubarikiwe sana,watumishi tusio na mauzauza tunakimbiwa wanaenda kwa matapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…