Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Mzee Mayalla hata wewe muda sio mrefu utapigwa na huyu Kuhani Musa unayemtetea. Hao unaosema wanapigwa na wao huwatetea manabii wao kama hivi unavyomtetea Kuhani tapeli. Makuhani walikuwepo enzi za Musa huko halafu leo 2023 anajitokeza kuhani wa Kimara hushtuki?
 
Nakazia. Lakin yote haya kwa kuwa pesa ndio inahibiriwa kuwa ni kila kitu kwa mwanadam. Watu tuko busy kutafuta pesa kuliko kingine. Binafsi kuna wakat huwa nazilaum sana Media zetu maana zimeweka pesa mbele zaidi kuliko kuangalia Athari ya kitu wanachoruhus kifanyike. Na ndio zinasababisha upuuzi huo unaenea Tanzania nzima.
 
Naunga Mkono Hoja hii

Hawa Manabii wafutwe au wafungiwe wote kwasababu ni MATAPELI na wanawafilisi Wananchi Masikini

Na hawa Wananchi ni Wajinga ndio maana wanaliwa
 
Serikali itawajuaje hao Manabii ni feki na wa uongo?

Ikumbukwe kuwa wapo Manabii wa kweli...

Hii hoja bado haitaweza kufanyika maana imegusa imani za watu...
 
Wajinga ndio waliwao! Sio kila kitu serikali upumbavu wa hao wanaotoa hela unataka uipe jukumu serikali kuingilia kati kwamba serikali haina mambo ya maana ya kufanya!?
Kwani wanalazimishwa kwenda huko,mbona makanisa yako mengi sana...
 
Acha Ujinga ww umesha kua msukule tayari hakuna vifaa vya kiroho huo ni utapeli.Shituka kabla giza halija tanda.
 
Mkuu, wote hawa baba yao ni mmoja.
Sioni hawa makuhani kama wako nje ya mfumo.
Rejea UKABAILA mmiliki wa mali mkubwa na mifumo yake
 
Njoeni kwenye dini ya haki, dini ya kweli (Uislamu) kabla milango ya toba haijafungwa.
 
Serikali haiwezi kuingilia uhuru wa kuabudu. Acha waendelee kupigwa maana ni wabishi sana
 
Hii mpaka alizwe mke wa kigogo ndipo watazinduka, mnakumbuka kipindi fulani watu walikuwa naporwa sana na majambazi Morogoro na serikali ikawa kimyaaaa mpaka alipofanyiwa uhalifu mke wa kigogo mmoja sikumbuki ni nani yule ila moto uliwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…