Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Serikali na hao manabii hawatofautiani, wote ni magenge ya wapiga dili kwaio hawawezikuingiliana katika ulaji, kikubwa elimu ya kujitambua.
 
Kutapeliwa kiimani unakuthibitisha vipi, kama ni muujiza utaambiwa muujiza wako bado, endelea kutumia mafuta na blahblah zingine.
 
Paskali ushapigwa ganzi na kuhani musa, haiwezekani umtete wakati yeye kabadili style ya kuwapiga wajinga?
 
Waache wachunwe wasije singizia seikali inawazuwia kwenda mbinguni,hawawatu wana akili na utashi ila wanadanganywa kwa tamaa zao nafikiri waachwe waingie ngomani was cheze
 
wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.
Hao watumishi wezi waliibuka kwa kasi kwenye awamu ya nne, binafsi naamini kuwa hao matapeli ni chimbuko la CCM, ongea yao, ushawishi wao wa kutapeli upo sawa sawa na ule wa wanasiasa hasa walioahidi MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ahadi ambayo haijawahi kutimizwa tunakatwa kodi nyingi sana.

Ishauri serikali ishughurike kwanza na hao wanasiasa waongo na matapeli waliojilimbikizia mali kwa njia ya utapeli huku wakitoa ahadi hewa ili wapate kura kubaki kila ufanyikapo uchaguzi.

Hao wanasiasa ni matajiri kuliko hata hao ma pastor,hivyo ma pastor wasishughurikiwe kabla wanasiasa wezi na waongo hawajashughurikiwa.
 
Sisi tunaomshabikia Jinping unatusoma wapi huko kwenye kuoshwa bongo ndugu?

Huko ni kwenu na nduguzo!

Nyie mnamshabikia muarabu, halafu huyo Mchina huwa namkubali sana kwenye kupiga mazombi ya dini yenu, kwake huko hamna hizo shobo zenu.

Nyie mlishavurugwa....

 
Serikali haiwezi kuingilia uhuru wa kuabudu. Acha waendelee kupigwa maana ni wabishi sana
Exactly my sentiments.

Njia pekee ya serikali kuingilia ni kuboresha elimu na huduma za umma.

Zaidi ya hapo serikali itaanza kuingilia uhuru wa watu kuabudu, jambo ambalo ni haki ya kikatiba (Freedom of worship, freedom of conscience, freedom to self determination) na haki ya kiutu, imeandikwa katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Tanzania imetia saini mikataba hii ya kimataifa ya kuheshimu hizi haki.

Yani mtu akitaka kupigwa na Mchungaji wake, hiyo ni haki yake ya kikatiba, utamzuia vipi hapo sasa?

Utasema asiamini katika Mungu wake na Mchungaji wake anavyotaka?

Huwezi.
 
Kati ya Manabii wa Uongo wa wazi wazi ni Nabii Dominic Kiboko ya Wachawi kutoka Buza kwa Lulenge ,huyo jamaa ana kipindi kila siku usiku Furaha FM ,watu wanapiga simu na anawaombea na kupona ,yaani yeyote ambaye anapiga simu hata awe na ugonjwa gani basi lazima apone....Cha kushangza tone na mtiririko wa wanaopiga simu hata akiongea kwa sauti tofauti basi lazima flow ziwe zinaendana.

Anawasisitiza ikifika saa 12 asubuhi usipige simu bali uende kanisani kwake Buza ,hiyo simu muda wote ipo busy means hao wanaopiga simu inaonekana wanarekodi kabisa mchana halafu usiku kipindi kinarushwa as if msikilizaji unaweza kujua wanapiga simu live kumbe ni recorded ,inaonekana kipindi kikiwa hewani huenda simu anaweka busy ili msikilizaji ambaye haujapangwa ukipiga usiipate.

Kuna siku mama mmoja alipiga simu mwanae amefariki cha kushangaza Nabii Dominic akamfufua ,aiseee watu wana utani sana.
 
Nyie mnamshabikia muarabu, halafu huyo Mchina huwa namkubali sana kwenye kupiga mazombi ya dini yenu, kwake huko hamna hizo shobo zenu.

Nyie mlishavurugwa....


1. Kung'ang'ania kuwalazimisha watu dini ni zaidi ya u zombie.

2. Waungwana hatujinasibu kwa dini bali kwa haki na usawa.

3. Ndiyo maana wemgine sisi wote ni wetu wakristo, waislam, wayahudi, banyan, Buddha na hata wapagani.

4. Kuwa tuna tatizo na mtu mmoja mmoja au kundi lililojinasibu wazi na hayo ya kibaguzi linayodai.

5. Waungwana sisi hatuna taabu na wayahudi wapenda haki na usawa kama kina Shimmon Perez, Ytzhak Rabin; lakini si Natenyahu, Ariel Sharon au Gallant.

6. Tuwe na taabu vipi na muyahudi mpenda haki na usawa - mbuzi wewe uliyeoshwa bongo!

7. Tuwe na suluhu vipi ni muyahudi kaburu!

8. Angalizo dini si 2 yaani ukristo na uislamu tu.

9. Ujinasibu na Xi wapi weye? Wacha urongo!

Bure kabisa!
 
Kutoa pesa wañatoa kwa hiyari yao hawajalazimishwa
 

Sasa hizi nadharia unaandika andika jihubirie na uhubirie mazombi wenzako, kama hawa waliochinja Wakenya kisa hawaabudu huyo muarabu wenu, wanateka bus na kuanza kuhoji kila asiyeabudu huyo muarabu halafu wanamchinja
 
Hapo ni pagumu
 
Kitu kikubwa kabisa hapo ni kufufua mtu, jambo ambalo Biblia imesema kwamba wafuasi wa Yesu watapewa uwezo wa kufufua watu.

Kwa hivyo huyo nabii akidai amefufua mtu, hakuna kitu chochote ambacho anasema yeye ambacho hakipo katika Biblia.

In fact, katika Ukristo, wewe unayehoji ndiye unaonekana kuwa wa imani haba, sasa huamini maneno ya Biblia kwamba kuna watu wanaomfuata Yesu watapewa vipawa vya kufufua watu?

Mimi nisiyeamini Mungu wala Ukristo nina haki kabisa ya kuhoji hizi habari. Ukishaamini Ukristo, wigo wako wa kuhoji unapungua sana, haya ni mambo ambayo yalisemwa katika Biblia, utashangaa vipi vipawa vilivyosemwa katika Biblia vikitimia?

Matthew 10:8
New International Version
Heal the sick, raise the dead, cleanse those who have leprosy, drive out demons. Freely you have received; freely give.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…