Serikali iingilie kati Suala la Bodi ya Mikopo. Ni Kama wamefanya makusudi maombi yashindikane

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
Habari wadau.

Naongea na watu wa bodi ya mikopo HESLB. Vijana wetu wanaenda kuomba mikopo kwenye website yao na hakuna msaada. Kwa mfano wamehitaji namba ya NIDA kwa hawa vijana. Baadae wanasema ni lazima Ufanye attachment ya kitambulisho cha NIDA.

Watanzania kibao wana namba. Ok basi itokee utake ufafanuzi hakuna namba inayopatikana. Wameweka kama geresha tu.

0736 66 55 33 (WhattsApp); 022 550 7910 (Calls from any network); adcp@heslb.go.tz. mawasiliano yao walio andika kwenye website haya lakini piga uoone utaacho kutana nachoo si whatsapp si regular call

Baadhi ya namba nyingine za landline tunaambiwa mtumiaji hajalipia. Kwa style hii wapeni tu wanenu mikopo.
 
Hii bodi ni mateso kwa watoto wa wanyonge kupata ukombozi kwa kupitia maarifa yatokanayo na kupata elimu ya chuo kikuu. Nilishashauri hii bodi ifutwe ili utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi waliodahiliwa vyuo vikuu vya umma urudishwe wizarani. Au laa hii bodi ibaki kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu binafsi ili kuwapa mwanya watoto wa wanyonge ambao wamepata nafasi kusoma vyuo vikuu vya umma wapewe ufadhili na serikali maana hivyo ni vyuo vya umma na vinaendeshwa kwa kodi za wananchi.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…