SoC04 Serikali ije na mikakati ya kutetea haki za makundi maalumu

SoC04 Serikali ije na mikakati ya kutetea haki za makundi maalumu

Tanzania Tuitakayo competition threads

west9

Member
Joined
Nov 27, 2018
Posts
19
Reaction score
9
UTANGULIZI
Kama ilivyo duniani kote, Serikali ni mfumo wa Mamlaka unaoongoza wananchi. Serikali zote duniani ndiyo huwa na Mamlaka ya nini kifanyike na nini kisifanyike nchi husika kwa kutunga Sheria. Kabla ya Sheria kuwepo, muswada hutungwa kupitia Bunge na kupitishwa ili kusainiwa na Rais na kuwa sheria kamili na Mahakama hupewa kazi ya kutafsiri na kutekeleza Sheria husika. Tanzania inaongozwa na mfumo wa Sheria. Sheria zote za nchi ya Tanzania zipo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ambayo hufanyiwa marekebisho kwa kupitiwa mara kwa mara kuhakikisha kuwa ina akisi sera za kidiplomasia kulingana na wakati uliopo.

Rejea na kichwa na andiko hili, wahusika wa makundi tajwa hapo juu wameongezeka na kuwa sio makundi maalumu tena bali ni raia wa Tanzania kwa pamoja kama walivyo raia wengine na serikali ndiyo mlezi wa raia wote.

Tumeshudia makundi maalumu yakiongezeka kama ifuatavyo:

  • Ongezeko la wapenzi wa jinsia moja:Ni dhahiri kwamba Serikali ya Tanzania haitambui haki juu ya wapenzi wa jinsia moja lakini andiko hili linatoa taarifa juu ya ongezeko la kundi hili. Madhara ya ongezeko ya kundi hili yamekuwa makubwa katika maisha yao kielimu,kiuchumi, kisaikolojia na kijamii. Makundi mengine yamekuwa yakiongelewa kwa muda mrefu lakini umefika wakati wa serikali kuangalia upya jambo hili na kufanyia kazi taarifa zinazotolewa nchini. Ongezeko la kundi hili linadhirika vyuoni, kazini,shuleni na majumbani. Andiko hili sio la wanaharakati ila linaelezea ongezeko kubwa la kundi hili licha ya kuwepo kwa sheria za nchi ambazo haziruhusu vitendo hivi.

  • Ongezeko la Watoto wa mitaani na kukosa haki zao kama matunzo kutoka kwa wazazi wao: Watoto ni Malaika, hawana makosa kwa kuzaliwa. Ongezeko hili linasababishwa na kukosa malezi kutoka kwa wazazi wao, mtoto anakosa chakula bora, elimu, na malezi stahiki. Hivyo wanaongezeka mitaani, wanakosa maadili mema na kukosa dhumuni la Maisha. Licha ya kwamba kuna sheria za kumlinda mtoto hapa nchini lakini bado kuna ukatili unaendelea dhidi ya Watoto kama kufanyishwa kazi, kunyimwa haki ya elimu na kunyanyaswa kijinsia.

  • Ongezeko la wanawake wanao dhulumiwa haki zao: Wanawake wamekuwa wakidhulumiwa haki zao kwa muda mrefu. Mwaka 2022 ilifanyika sensa nchini, idadi ya wanawake imekuwa kubwa kuliko wanaume. Tamaduni nyingi za makabila hapa nchini haziwapi wanawake kipaumbele. Bado Wanawake wanazuiwa kumiliki ardhi,kufanya kazi, kupewa urithi, kuzuiwa kwenda shule, mimba za utotoni na kukeketwa kwa baadhi ya jamii. Hii inapelekea matatizo kiafya,kielimu na kisaikolojia. Azimio linaloelezea maoni juu ya haki za wanawake lilipitishwa na Umoja wa Mataifa mnamo 07/11/1967, Sheria za kumlinda mwanamke zipo muda mrefu hapa nchini lakini ukatili dhidi ya wanawake unaendelea kama unyanyasaji wa kijinsia na kunyimwa fursa ambazo wanaweza kuzifanya kama wanaume. Ibara ya 22(1) ya Katiba inaelezea.View attachment 3008825Imetolewa:Msajiri wa Vyama Vya Siasa

  • Ongezeko la walemavu na wazee ambao wanakosa matunzo: Walemavu wameongezeka nchini hasa katika majiji kama Dar Es Salaam na Dodoma. Wazee wameongezeka vijiji vya mikoa kama Rukwa, Lindi na Iringa vinaongoza. Serikali imekuwa ikilizingatia kundi hili kwa muda mrefu lakini bado inazidiwa.

  • Ongezeko la vijana wasomi na wasio wasomi waliokosa ajira nchini: Vijana ni Taifa la kesho, ongezeko la vijana wasomi na wasio wasomi wasio na ajira limekuwa kubwa hivyo kupelekea kujiingiza katika uhalifu, ulevi na biashara haramu. Vijana wakike na wakiume wamepoteza dira ya maisha, hii ni hatari kwa ustawi wa nchi. Serikali inawasaidia vijana kwa muda mrefu kwa kutoa elimu na mitaji lakini bado inazidiwa.

Ushauri kwa Serikali juu ya ongezeko la makundi maalumu:

  • Serikali iangalie upya jinsi ya kuwasaidia wapenzi wa jinsia moja: Serikali isaidie kundi hili katika nyanja zote kielimu, kiafya na kijamii na kisaikolojia, jamii ikanywe kuhukumu wengine. Sheria kandamizi dhidi ya kundi hili ziangaliwe upya. Serikali iweke mipango ya kutenga bajeti juu ya kundi hili kwa kushirikiana na wadau mbali mbali na asasi za kiraia kama Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali (au NGO's).Watoto wadogo walindwe kwa Sheria kuwanusuru.Ibara ya 12(1) ya Katiba inaelezea haki ya usawa.View attachment 3008826Imetolewa:Msajiri wa Vyama Vya Siasa
  • Uhuru Wa Vyombo Vya Habari:Vyombo vya Habari vitumike kutoa taarifa kufikia jamii yote kadri ya mahitaji.View attachment 3008833Imetolewa:ICNL, Ibara ya 18 ya katiba
  • Serikali iweke mikakati mipya ya kusaidia ongezeko la Watoto wa mitaani: Kupitia serikali na wadau elimu ya uzazi itolewe. Wazazi wajipange kabla ya kuzaa watoto.Sheria ziimarishwe dhidi ya Watoto.View attachment 3008830Imetolewa:Tume Ya Kurekebisha Sheria, Sheria ya mtoto
  • Serikali iweke mipango zaidi ya kuwezesha wanawake: Wanawake wasomi wamekuwa wengi nao wawekewe vipaumbele katika ajira, hata viongozi wa juu wa Nchi ni Wanawake kama Rais wa nchi, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge, Dr Tulia Ackson na Waziri wa Ulinzi, Dr Stergomena Tax. Wazazi wawekeze kwa Watoto wote kwa usawa. Madawati ya jinsia yaweke mikakati ya kuwezesha kupatikana kwa haki za wanawake na Watoto kama mirathi na matunzo. Vipaji vya wanawake vikuzwe kama mpira, fashion na muziki.View attachment 3008827Imetolewa: IKULU:Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu​
  • Serikali iweke mikakati mipya ya kuwezesha walemavu na wazee: Mikakati mingi imefanywa na serikali kupitia mashirika mbalimbali kama Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) toka kuanzishwa kwake mwaka 2000 kuwezesha kaya maskini kuongeza kipato na kuboresha matumizi. Lakini kwakua hali ya maisha inaenda kupanda baada ya muda fulani, serikali iweke mikakati kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga vituo vya kulelea wazee na walemavu ili kulinda kundi hili ili wahisani na raia wengine waisaidie serikali. View attachment 3008837Imetolewa:TASAF, Mnufaika WA TASAF
  • Serikali iruhusu wawekezaji wengi na biashara ya soko huria ili kuajiri vijana wengi waliokosa ajira: Kuruhusu wawekezaji ni kuruhusu mitaji kuingia nchini na Uchumi kukua na kuajiri kundi kubwa la vijana. Sheria za kodi na michakato ya kusajiri biashara iwe wazi ili vijana nao waweze kujiajiri wakiweza.Vijana nao wajiulize wameifanyia nini Tanzania.
  • View attachment 3008829Ujenzi wa kituo cha masoko,Ubungo​
  • Imetolewa: EATV, Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums Bwana Maxence Melo​

HITIMISHO
TANZANIA TUITAKAYO:
Ni ni ile yenye Raia wenye tabia kama za paka ambapo hulia kwa mmiliki wake akiwa na shida tu na sio kuwa na tabia kama za mbwa ambapo huwa mnafiki kwa kumlilia mmiliki wake hata kama hana shida pamoja na kumsaliti licha ya kutendewa mema. Tulalamikie SERIKALI pale tu inapobidi. Pia nawapongeza sana JamiiForums na Shirika la TWAWEZA kwa kuweza kusaidia serikali katika kuibua kero na kuwezesha uwajibikaji nchini na nchi Jirani.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom